31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

BIASHARA NI VITA AFRIKA IAMKE – 5

OR Book Going Rouge

Na Markus Mpangala,

TUNAENDELEA na sehemu ya tano na ya mwisho ya kitabu hiki cha “Trade Is War: The West’s War Against the World” kilichoandikwa na Yash Tandon na kuchapwa na Kampuni ya Mkuki&Nyota.

Tunakumbuka kwenye mkutano wa WEF (World Economic Forum) pale Mlimani City jijini Dar es salaam, miaka ya nyuma Rais Mstaafu Benamin Mkapa, alitoa hotuba kali kuzionya nchi za Afrika juu ya mkataba wa EPA.

Yawezekana Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alisoma mchezo pia, akazipiga kalenda. Maelezo hayo yanapatika katika ukurasa wa 73 wa kitabu hiki ambapo mwandishi ameyapa kichwa cha habari “How the people of east Africa trounced the Economic Commissin,’ Dar es salaam.

Aidha, anatukumbusha namna timu ya ushawishi zilivyotua Dar es Salaam kwa minajili ya kusisitiza mkataba wa EPA. Na jinsi mji huo ulivyogeuka kuwa kituo cha mapambano ya ushawishi wa kusaini EPA.

Sasa tujiulize swali; hivi kulikuwa na masharti gani ambayo yalisababisha kuonekana EPA kama mkataba mbaya na usio na masilahi kwa Tanzania pamoja na Afrika kwa ujumla?

Katika ukurasa 74 wa kitabu hicho wenye kichwa cha habari, “The seven most contentious issues in the EC-proposed text to the EAC on FEPA,”. Kama tulivyosema kabla ya EPA kulikuwa na FEPA. Kwahiyo haya ni masharti yake;

  1. Kupunguzwa ushuru wa bidhaa za nchi wanachama wa Jumuiya ya Ulaya kwa asilimia 80.
  2. Kuruhusu kuingizwa bidhaa kutoka Ulaya zenye thamani kubwa kwa asilimia 17.4 na kulinda soko lake.
  3. Kuleta chakula cha ziada kama kunatokea matatizo ya kisiasa kwa nchi za wanachama wa EAC.
  4. Kwa mujibu wa ibara ya 13 ya mkataba ilitaka kutoongezwa ushuru bidhaa za nje kwa miaka 25.
  5. Ibara ya 15 ya FEPA ongezeko la kodi katika usafirishaji wa bidhaa za EAC kwenda Ulaya halitaruhusiwa.
  6. Ibara ya 16 ya FEPA ilisema ushirikiano wowote kati ya nchi za EAC na China, India au Brazil ni lazima uzishirikishe nchi za Jumuiya ya Ulaya.

Mkataba huo haukuwa na masilahi kwa Tanzania kwa sababu kwanza tuko katika kundi la nchi zenye maendeleo hafifu. Nchi zilizopo kwenye kundi hilo zinapewa nafasi ya kipekee kwenye soko la Jumuiya ya Ulaya na Marekani pasipo zenyewe kutoa nafasi hiyo kwa nchi za Ulaya na Marekani.

Katika moja ya vipengele vya mkataba huo kilitaka kama nchi itapata hasara kwa kuingia mkataba wa EPA basi nchi hiyo ipandishe tozo ya VAT kufidia. Hii ina maana kwamba endapo tungeingia mkataba huo na kupata hasara ya kusamehe wao hiyo kodi basi wananchi wetu wabebe hasara hiyo kwa kuongezewa VAT.

Lakini je, ni kweli Kenya walihitaji mkataba wa EPA? Jawabu tunalopata ni hapana kwakuwa Kenya waliambiwa wasiposaini bidhaa zao zinazoingia EU zitatozwa kodi si chini ya asilimia 10. Tukitazama kwa mwaka 2015 tu bidhaa za Kenya zilizouzwa EU zilikuwa na thamani ya dola bilioni 1.5 ndiyo kusema kama wangetozwa kodi wangetakiwa kulipa dola milioni 150.

Pia katika bidhaa ambazo Kenya wanapeleka EU ni kwamba asilimia 28 zinakwenda Uingereza, kwahiyo tunaona pia faida ya Kenya kwenye soko la Ulaya limepungua kwakuwa Uingereza imeshajitoa EU, tofauti na upande wetu wa Tanzania ambapo tulihitajika kuukataa mkataba huo.

Kwa mantiki hiyo maneno matamu ya washawishi waliotaka tusaini mkataba wa EPA hawakuona ukweli kuwa tunaua viwanda vyetu tunavyotarajia kuvijenga. EPA ingetufaa kama tungekuwa na nguvu kwenye sekta ya viwanda na uzalishaji mkubwa wa bidhaa.

Tafsiri tunayoipata kwenye kitabu hiki ni kwamba serikali yetu inatakiwa kujipanga kuimarisha sekta ya viwanda kwa sababu baada ya miaka 10 nina uhakika hatutobaki kundi la nchi masikini zaidi (LDC).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles