27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

BIASHARA MBOGAMBOGA TANZANIA YASHAMIRI

Na Mwandishi Wetu-ARUSHA

MKUTANO wa kimataifa wa siku mbili kuhusu biashara na kilimo cha mbogamboga, umemalizika kukiwa na habari njema kwa Tanzania kuahidiwa kupata msaada wa kuendeleza kilimo hicho.
Mtaalamu Mkurugenzi na Mtafiti mahiri wa Korea Kusini, Ji Geng Kim, anasema nchi yake itaisaidia Tanzania katika kilimo cha mbogamboga na matunda (horticulture) kwa kuipa teknolojia ya kisasa ili mavuno yao yote yaweze kutengenezwa vizuri na kuongezwa thamani ili kuvutia masoko mazuri ya  nje na kupata faida kubwa.

“Kinachotakiwa ni kufanya mapinduzi makubwa ya kilimo hicho na teknolojia hiyo itaoneshwa katika maonesho maalumu, jijini Dar es Salaam wiki ijayo,” anasema Kim.

Korea Kusini inazalisha zaidi ya tani milioni 10 za mbogamboga wakati Tanzania inazalisha tani milioni sita tu na hivyo, kuna nafasi kubwa kwa nchi hii kuongeza kilimo hicho pendwa katika masoko ya kimataifa kadiri ya watu wanavyobadilika kwa maendeleo na kutaka kula vyakula vyenye faida ya afya kwa mwili na hivyo kupunguza magonjwa.

Wadau wa kilimo cha mbogamboga na matunda 200 kutoka sehemu mbalimbali duniani, wiki jana walikutana jijini Arusha na kujadili kwa pamoja changamoto zinazoikabili sekta hiyo na baadaye kupata wasaa wa kutembelea maeneo mabalimbali ya kilimo hicho.

Wadau hao walitoka nchini na Korea Kusini, Burundi, Rwanda, Nigeria,

Tanzania Horticulture Association (TAHA) ni taasisi mujarab inayoshugulikia masuala ya mbobamboga nchi nzima na imefanikiwa sana kwa hilo na kufanya mauzo ya mwaka jana kufikia dola milioni 640 na kuzidi mauzo ya mazao yote ya asili (traditional crop) ikiwamo kahawa, chai  na tumbaku na iko chini ya uongozi mahiri wa Mkurugenzi Mtendaji, Jaqueline Mkindi.

Akiongelea mafanikio ya Taha, Jaqueline anasema sekta ya mbogamboga iko imara katika lengo lake la kufikia mauzo ya dola bilioni 1.3 katika mwaka huu hadi ujao na kufikia lengo kuu la kupata dola bilioni 2, baadaye ili kuipiku sekta ya utalii kama kinara wa kuleta fedha za nje nchini.

Kwa niaba ya mgeni mwalikwa Waziri wa Kilimo, Dk. Charles Tizeba, kwa niaba yake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Mkalla, alisema sekta ya mbogamboga hutoa mapato yafikiayo asilimia 43 kutoka kilimo na huajiri zaidi ya watu milioni 2.5 na hivyo lazima itiliwe mkazo kwa uchumi wa nchi hii.

Meneja Maendeleo wa Taha, Anthony Chamanga, alisema kufanyika kwa mkutano huo hapa nchini ni matokeo ya kazi nzuri inayofanywa na tasisi yake katika kukuza na kuendeleza sekta hiyo.

Alisema katika mkutano huo, wadau hao walijadili na kubadilishana uzoefu hususan namna ya kuandaa mashamba, mbinu bora za kilimo, upatikanaji wa pembejeo, mabadiliko ya tabia nchi na upatikanaji wa masoko ya uhakika.

“Katika mkutano huo ambao ulihusisha wataalamu, wanasayansi, wakulima, wafanyabiashara na wadau wengine wa sekta hii ya mbogamboga kutoka kila pembe ya dunia.

Chamanga alisema lengo lao Taha ni kuhakikisha mkulima mdogo wa nchi anapata tija katika kazi yake ndio  maana walialikwa  ili waje wajifunze namna ya kutumia teknolojia ya kisasa katika shughuli zao.

Naye Jaqueline alisema kwa muda mrefu, Taha imekuwa ikihimiza wawekezaji wa ndani katika sekta ya kilimo cha mbogamboga na matunda hususan eneo la pembejeo za kilimo na viwanda vya kusindika mazao hayo kisasa.

“Tunataka uwekezaji wa uhakika ufanyike, wananchi na hasa wakulima waache kilimo cha mazoea kwa kuwa wabunifu.”

Wachunguzi wa mambo wanasifia utendaji kazi wa Taha na kutaka Serikali iwaunge mkono kwa hali na mali.

“Kuna mazao zaidi ya 200 katika sekta hii ndio maana tunaandaa mikutano ya aina hii ili waje wajifunze na wabadilishane uzoefu,” alisema Chamanga.

Aidha, mkutano huo ulielimisha wananchi namna ya kutumia mbogamboga, matunda na viungo kama tiba mbadala ya magonjwa yanayosababishwa na ukosefu wa lishe bora.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles