Biashara 16,000 zimefungwa ndani ya mwaka mmoja

0
586

Arodia Peter, Dodoma

Naibu waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji amesema biashara zilizofungwa kuazia Julai mwaka jana hadi Aprili mwaka huu ni 16,250.

Dk Kijaji amesema licha ya hilo, biashara mpya zilizofunguliwa zimefikia 147,818.

Akifafanua hoja mbalimbali za wabunge leo, Mei 15. amesema wafanyabiashara halali wanaendelea kufanyabiashara vizuri na uchumi wa nchi uko salama na makusanyo ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hayajawahi kushuka chini ya Sh trilioni moja kwa mwezi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here