27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

BESIGYE AMTUHUMU MUSEVENI KUHONGA WAPIGAKURA

KAMPALA, UGANDA


ALIYEKUWA mgombea urais wa Chama cha Forum for Democratic Change (FDC), Dk. Kizza Besigye, amewaambia wafuasi wake kuwa Rais Yoweri Museveni anatumia kodi zao kuwahonga wapigakura.

Akimpigia kampeni mgombea wa FDC, Robert Onega, kuwania ubunge katika uchaguzi mdogo wa Manispaa ya Nebbi, Besigye alidai umasikini na ukosefu wa ajira umesababishwa makusudi na vitu vinavyopandikizwa na Serikali ya NRM ili kuwakatisha wananchi tamaa.

“Mabilioni ya fedha za walipakodi yanatolewa kwa watu kama rushwa ili kuwapigia kura wagombea wa NRM, huku barabara na hospitali zetu zikihitaji sana fedha hizo kuziboresha,” alidai.

Kwa mujibu wa Besigye, Uganda ilikuwa nchi tajiri kabla ya NRM kuingia madarakani mwaka 1986, lakini sasa kila kitu kinaibwa na Serikali ya NRM na kuiacha nchi nzima masikini.

Shughuli za biashara zilikwama kwa saa moja wakati maelfu ya wafuasi walipojitokeza katika msafara wa kumpokea Besigye na timu yake kwenye Bustani ya Meya wa Nebbi, ambako mkutano wa hadhara wa Onega ulifanyika.

Rais wa FDC, Patrick Amuriat, aliwataka wapigakura wa Nebbi kumpiga kura mgombea bora, ambaye atafanya kazi bila kuchoka kuleta mabadiliko katika eneo lao.

Alisema vyama vya upinzani ni sauti ya jamii zisizosikika na hivyo zipewe mamlaka kwa sababu wana uwezo wa kuleta mabadiliko haraka nchini.

Kwa upande wake, Onega aliwataka wafuasi wake kuwa watulivu na kuepuka siasa za utengano, ukabila na machafuko.

Aliongeza kuwa amelenga kuwaunganisha wapigakura wa Manispaa ya Nebbi kufanya kazi kama timu moja ili kuchochea maendeleo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles