23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Benki ya Posta yaahidi kuwaunga mkono wakulima Lindi

Hadija Omary, Lindi

Benki ya Posta Tazania (TPB), Mkoa wa Lindi imesema itaendelea kuwaunga mkono wakulima wa Mkoa huo moja kwa moja katika kuwapa mikopo ya pembejeo isipokuwa wakulima wa bangi.

Hayo yameelezwa na Meneja wa benki hiyo Fluence Mushi, alipokuwa anatoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu juu ya namna benki hiyo inavyoshiriki katika kuwasaidia wakulima wa Mkoa huo katika maonyesho ya wakulima nane nane kanda ya Kusini  katika Viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi yanayoendelea hivi sasa.

Amesema kwa kutambua Shuguli zinazofanywa na wakulima benki hiyo imeamua kutoa mikopo ya pembejeo na matrekta kwa wakulima yenye lengo la kuwasaidia kuongeza tija ya uzalishaji katika kilimo chao.

Amesema kuwa wanazo akaunti maalumu za wakulima ambazo wanazifungua kwa masharti nafuu bila kuhitaji picha wala fedha za kuanzia, lengo likiwa ni kuwafanya wakulima walio wengi kufungua akauti ili kufanya usalama wa fedha zao wakati wa mauzo ya mazao yao.

Akizungumza mara baada ya Kupata maelezo hayo kutoka kwa Meneja wa benki hiyo Naibu waziri Kunyusa, aliushauri uongozi wa benki hiyo kulegeza baadhi ya masharti wanayoyaweka katika uchukuwaji wa mikopo ili kutoa fursa kwa wakulima walio wengi kuweza kukopa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles