30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

BENKI YA DUNIA YAIPA TANZANIA MKOPO WA TRILIONI 1.8

Na Mwandishi Wetu-Dar es Salaam


Benki ya Dunia (WB), imeipatia Tanzania mkopo wa masharti nafuu wa Sh trilioni 1.8 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi wa nishati na maji nchini.

Akizungumza le jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James, alisema kuwa mkopo huo wa masharti nafuu utakuwa na manufaa kwa nchi.

Alisema katika fedha hizo Wizara ya Nishati kupitia Tanesco itapewa Sh trilioni 1.04 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa umeme unaounganisha Tanzania na Zambia na sehemu ya Magharibi mwa nchi.

“Na upande wa maji wao watapata Sh bilioni 800 ili kuweza kutekeleza miradi ya maji vijijini. Kwa mjini maeneo mengi tumefanya vema na sasa serikali kupitia Hazina kazi yetu ni kutafuta fedha kama hivi ili kuweza kufikia malengo ya serikali na kutekeleza miradi ya maendeleo,” alisema James.

Pamoja na hali hiyo, alisema kwa sasa serikali imedhamiria kusimamia kwa vitendo utekelezaji wa miradi yote ya maendeleo kama ilivyopangwa.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo, alisena fedha hizo zinakwenda kutekeleza miradi kwenye mikoa 17 kwa kuimarisha huduma za maji, vyanzo.

“Pia fedha hizi zitakwenda kuimarisha taasisi zinazozimamia vyanzo vya maji pamoja na kuimarisha usafi ikiwamo zahanati na shule kwa kuwa na maji ya uhakika,” alisema Profesa Kitila

Alisema anaishukuru serikali kupitia Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, ambaye akuwa akitafuta fedha za miradi ya maji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles