24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

BENCHI SI DHAMBI, LAKINI JONAS MKUDE MH MH..!

Na ZAINAB IDDY-DAR ES SALAAM


HIVI sasa wanachama, mashabiki na baadhi ya viongozi wamekuwa na sitofahamu juu ya nahodha wao wa zamani Jonas Mkude, ambaye anaonekana dhahiri, hana nafasi ndani ya kikosi cha kocha Joseph Omog.

Mkude akiwa ndiye kiungo mzoefu ndani ya Simba, aliyeanza kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara mwaka 2012, akitokea kikosi cha pili cha timu hiyo, kilichokuwa kikifundishwa na kocha Seleman Matola.

Inakumbukwa tangu alipoanza kuitumikia Simba, Mkude ameonekana ndiye kiungo bora wa muda wote, jambo lililowashawishi Yanga kuingia katika mipango ya kumsajili msimu huu, kabla ha Simba kutumia mbinu na maarifa ya kumbakisha kwenye timu yao.

Licha ya kutumia nguvu na fedha nyingi kumbakisha, lakini anaonekana hana nafasi katika timu hiyo, huku nafasi yake ikionekana kumilikiwa vilivyo na James Kotei rai wa kigeni.

Hapo ndipo sitofahamu inapotawala katika vichwa vya wanamichezo wengi, kwani uwezo wa Kotei unaonyesha dhahiri hauwezi kumuweka Mkude benchi.

Si dhambi Mkude kukaa benchi, lakini zipo sababu zinazomchomesha mahindi? Je kiwango chake kimeshuka, hayupo kwenye mipango ya kocha, nidhamu mbovu au kunanini nyuma ya panzia? majibu ya maswali haya anayo kocha Omog pekee.

Lakini iwapo kama hayupo katika mipango ya kocha kwanini alisajiliwa, je nani aliyependekeza apewe mkataba mpya ni Omog au viongozi wa Simba, sababu zipi za kubakishwa kwake? kiukweli Mkude bado yupo katika kiwango bora uwanjani na hakika kama atapewa nafasi anauwezo wa kuisaidia timu.

Ukweli Mkude bado yupo katika kiwango bora uwanjani na hakika kama atapewewa nafasi anauwezo wa kuisifia timu. Hakuna asiyejua kuwa msimu huu Simba inahitaji kukata kiu waliyonayo ya kutwaa ubingwa na Mkude ni mchezaji sahihi, mwenye kiu ya kuipa Simba inachotaka.

Kitendo cha Omog kumuweka benchi Mkude kinazua maswali mengi yasio na majibu, yanaweza kuja kumgharimu Mcameroon huyo.

Ni wakati wa Omog kumtumia Mkude au aweke wazi kipi kinachosababisha asipewe nafasi, kwenye mechi zote nne za Ligi Kuu iliyocheza timu hiyo.

Zipo taarifa nyingi zinapenya katika masikio ya wadau wa soka juu, kubwa ikiwa ni nidhamu mbovu na kutoelewana  viongozi wa benchi la ufundi.

Suala la nidhamu mbovu kwa Mkude naweza kukubaliana nalo kwani si mara moja kiungo huyo ameonekana akichelewa mazoezini, lakini mbona licha ya jambo hilo anaonekana anakiwango cha ushindani kuliko Kotei anayeaminiwa na Omog?.

Si dhambi Mkude kukaa benchi, lakini zipo sababu zinazomchomesha msingi au ndo kusema Mkude ni mchezaji wa mechi za kirafiki pekee na si za Ligi Kuu?.

Kama ndio, Omog weka wazi ili kujioendolea kuvaa mizigo ya lawama, ambayo uenda austahili kubeba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles