33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Beki Mniger atua majaribio Azam

Na ADAM MKWEPU – DAR ES SALAAM

KLABU ya soka ya Azam FC inaendelea kujiimarisha katika mchakato wa usajili kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao, baada ya kumleta beki, Chicoto Mohamed, raia wa Niger kwa majaribio

Chicoto alitua nchini juzi akitokea katika klabu ya ASM Oran ya Algeria ambayo aliichezea msimu uliopita.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Ofisa habari wa klabu hiyo, Jaffar Idd, alisema beki huyo ataanza mazoezi rasmi leo chini ya kocha mkuu, Zeben Hernandez na iwapo atafuzu atasajiliwa kwa msimu ujao wa ligi.

“Kocha amepanga kufanya maboresho makubwa katika safu ya ulinzi na ushambuliaji ili kuimarisha kikosi, lakini hawezi kusajili mchezaji kwa kumwangalia usoni ndio maana wanaanza kwanza majaribio kupimwa uwezo walionao,” alisema.

Chicoto anayecheza katika kikosi cha timu ya Taifa, pia aliwahi kukipiga katika klabu ya Sporting Sahel ya Niger, Platinum Stars ya Afrika Kusini, AS Marsa ya Tunisia na Coton Sports ya Cameroon.

Mniger huyo anaungana na wachezaji wengine watatu wa kigeni ambao wanaendelea kufanya majaribio ambao ni Daniel Yeboah, Ibrahim Fofana kutoka Ivory Coast na Juan Jesus Gonzalez raia wa Hispania.

Hadi sasa wachezaji wa kigeni walioshindwa majaribio Azam na kuondolewa kwenye orodha ya usajili ni beki wa kushoto kutoka timu ya Medeama ya Ghana, Yusif Nurudeen na kiungo David Wirikom kutoka Cameroon.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles