BEKA AWACHIMBA MKWARA WASANII

0
692

NA BADI MCHOMOLO


MSANII wa muziki nchini, Beka Ibrozama, amechimba mkwara kwa wasanii mara baada ya kuachia video ya wimbo wake mpya ujulikanao kwa jina la Kangaroo.

Msanii huyo amedai baada ya kuachia video ya wimbo huo, sasa anakuja rasmi kwenye ushindani, huku tayari akiwa amekamilisha nyimbo tano ambazo zitatoka baadaye.

“Ni kweli nilikuwa kimya sana bro, lakini niwaambie mashabiki wangu kuwa, baada ya kuachia video yangu ya Kangaroo, sasa kinachofuata ni weka niweke.

“Kuna ushindani mkubwa kwenye muziki kwa sasa, hivyo lazima ujipange ili kuhakikisha unarudisha mashabaki wako, ninaamini mashabiki wangu wanasubiri kazi zangu, kwa hiyo wakae tayari,” alisema Beka.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here