25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

BAWASIRI: UGONJWA UNAOWEZA KUUPATA BAADA YA KUJIFUNGUA

 

 

BAWASIRI ni ugonjwa unaojitokeza katika njia ya haja kubwa, hujitokeza kama uvimbe au kijinyama ambacho huweza kuonekana hadi nje. Kwa Kiingereza ugonjwa huu huitwa Haemorrhoids au piles.

Bawasiri inaweza kusababisha upungufu wa damu mwilini lakini unaweza kutibiwa kwa njia ya upasuaji au kwa kutumia dawa mbadala kwa kipindi cha kuanzia  wiki sita na kuendelea, inategemea imejijenga kiasi gani.

Bawasiri husababishwa na nini?

Hakuna sababu ya moja kwa moja inayojulikana kisayansi kwamba ndiyo husababisha bawasiri, bali mambo yafuatayo yanaweza kukufanya ukapata ugonjwa huu:

  1. Kufunga choo au kupata choo kigumu kwa muda mrefu
  2. Ujauzito; wakati wa ujauzito watu wengine wanaweza kupatwa na bawasiri sababu ya msukumo wa mtoto karibu na sehemu ya kutolea haja kubwa.
  3. Kushiriki mapenzi kinyume na maumbile
  4. Uzee; kadri miaka inavyosogea ndivyo inavyokuwa rahisi kwako kupatwa na ugonjwa huu kwa baadhi ya watu.
  5. Sababu za kurithi; baadhi ya watu wanaweza kurithi udhaifu wa ukuta huo wa njia haja kubwa ingawa ni kwa asilimia ndogo.
  6. Kuharisha kwa muda mrefu.
  7. Kutumia vyoo vya kukaa.
  8. Kunyanyua vyuma vizito.
  9. Mfadhaiko
  10. Uzito na unene kupita kiasi.

Dalili zake

Ili  kujua kama una ugonjwa huu ni lazima utasikia maumivu wakati wa kujisaidia haja kubwa, kinyesi kunuka damu wakati wa kujisaidia.

Dalili nyingine ni muwasho sehemu ya tundu la haja kubwa, uvimbe au kinyama kujitokeza sehemu ya tundu la haja kubwa na haja kubwa inaweza kutoka bila taarifa muda wowote.

Matibabu kwa njia ya asili

Matibabu haya yanategemea na umri wa mgonjwa na namna ugonjwa ulivyojijenga na kudumu, unaweza kuhitaji dawa moja au mbili au hata tatu kwa pamoja kati ya hizi zifuatazo. Hivyo, kabla ya kuzitumia ni muhimu kumshirikisha daktari wa tiba mbadala au kwenda hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi ikiwezaka kufanyiwa upasuaji.

Habbat-Sawdaa

Chukua kijiko kikubwa kimoja cha unga wa Habbat-Sawdaa ukoroge ndani ya glasi moja ya  maji na unywe yote. Fanya hivi kutwa mara mbili kwa wiki mbili mpaka tatu hivi.

Habbat-Sawdaa na asali

Changanya gm 500 za unga wa Habbat-Sawdaa na nusu lita ya asali. Lamba kijiko kimoja kikubwa cha chakula kila baada ya saa nne. Ukimaliza kulamba kunywa glasi moja ya maji ya kunywa ya joto la kawaida.

Aloe Vera Fresh

Chukua kipande cha jani la mmea wa Aloe vera fresh (mshubiri) na kikate ukimenye kidogo ukitumia kidole kupata kama utomvu hivi au maji maji yake na upake sehemu ya utupu wako wa nyuma baada ya kuoga kutwa mara tatu.

Jipake nyingi tu na uiache hivyo kwa saa kadhaa au mpaka utakapaoenda kuoga tena.

Tengeneza pia juisi ya mmea huu na uchanganye nusu glasi dawa hii na nusu glasi nyingine ya juisi yoyote ya matunda uliyotengeneza nyumbani ili kupata glasi moja iliyojaa na unywe glasi moja kutwa mara mbili kwa wiki tatu hadi nne. Juisi ya aloe vera ni nzuri kwa kuongeza kinga ya mwili na kutoa taka zote za ndani ya mwili.

Unga wa Habat Sawda husaidia kutibu bawasiri

Juisi ya limao (lemonade)

Chukua juisi ya limau na upake sehemu iliyoathirika. Juisi ya limao sifa yake kuu ni kuondoa sumu na kuongeza kinga ya mwili kwa kuwa ina vitamin C kwa wingi. Pia unywe glasi moja ya juisi hii kutwa mara kwa wiki tatu hadi mwezi mmoja.

Lemonade inaandaliwa kwa kutumia limau na asali na mdalasini ya unga kidogo, nayo inaandaliwa hivi:

  • Chukua asali nusu lita
  • Chukua limau kubwa 12, zikate katikati kila moja.
  •  Tumbukiza ndani ya sufuria na weka maji lita tatu, chemsha mpaka limao ziive (zisiive sana), ipua utowe zile nyama nyama za ndani za liamau moja baada ya nyingine, ganda la nje tupa na uchuje kupata juisi ambayo itakuwa na ujazo wa lita 2 na nusu hivi.
  • Kwenye sufuria nyingine kubwa changanya ile asali nusu lita na hiyo juisi ya limau lita mbili na nusu, ongeza maji safi ya kawaida lita mbili ili kupata lemonade ya ujazo wa lita tano. Ihifadhi katika friji au kama huna friji andaa kiasi kidogo kidogo cha kutumia siku tatu kisha unaandaa nyingine.
  • Kunywa robo lita kutwa mara mbili kwa siku 10 hadi 11.
  • Unaweza kuongeza vijiko vikubwa vitatu vya mdalasini ya unga ndani ya juisi ya limao.

Siki ya tufaa

Chukua kipande cha pamba na ukichovye ndani ya siki ya tufaa (apple cider vinegar) na ujipake kidogo kidogo eneo lenye uvimbe taratibu. Unaweza kusikia maumivu zaidi lakini jipe moyo taratibu yatapotea. Hakikisha unapata siki ya tufaa ile ya asili kabisa si ile iliyopita viwandani.

Pia kama una bawasiri ya ndani yaani ile isiyojitokeza nje na ukaiona kwa macho moja kwa moja unashauriwa kuchanganya kijiko kidogo kimoja cha siki ya tufaa ndani ya glasi ya maji na unywe yote kutwa mara mbili. Hii husaidia pia kupunguzia maumivu.

Mafuta ya nyonyo

Pakaa mafuta ya nyonyo mara mbili mpaka tatu kwa siku sehemu ya utupu wako wa nyuma kwa wiki tatu hadi nne.

Mambo muhimu ya kuzingatia ili kuepuka bawasiri

Kuzingatia vyakula ni jambo la muhimu mno unapohitaji kupona ugonjwa huu. Mgonjwa anapaswa kula vyakula vingi vyenye faiba, kunywa maji mengi kila siku ili kusafisha mwili na kuepuka kufunga choo, kula mboga majani na matunda kwa wingi, tumia mafuta ya mzaituni (olive oil) kwa wingi kwenye vyakula na epuka kufanya mapenzi kinyume na maumbile.

Mwandishi wa makala hii ni Fadhili Paulo ambaye pia ni tabibu wa tiba asili, kwa mawasiliano tuma ujumbe mfupi wa maneno kupitia WhatsApp +255769142586.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles