33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Bashiru ataja matatizo matatu yanayovikumba vyama vya siasa

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam



Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally, ameorodhesha matatizo matatu yanayovitatiza vyama vya siasa nchini kikiwamo chama chake, kuwa ni kutokuwa na mtazamo wa pamoja kiitikadi, nidhamu na utegemezi.

Dk. Bashiru ameyasema hayo leo Ijumaa Oktoba 12, wakati akichangia mada katika mdahalo wa miaka 19 ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, ambapo mada kuu ilikuwa ni mienendo ya uchaguzi na mustakabali wa mataifa ya Afrika, ulioandaliwa na Kigoda cha Mwalimu Nyerere.

Katika suala la kutokuwa na mtazamo wa pamoja wa kiitikadi, Dk. Bashiru amesema chama kinapaswa kufahamu nini wanatakiwa kufanya, si kubishana wenyewe kwa wenyewe na hali hiyo ipo zaidi ndani ya CCM kuliko vyama vingine.

“Ndiyo maana tunasisitiza kuwa na mtazamo wa pamoja wa kiitikadi haki,” amesema.

Aidha, Dk. Bashiru pia amesema nidhamu ni moja ya matatizo aliyokumbana nayo ambapo kwa ujumla wake alisema vyama vingi havina nidhamu.

“Vyama vyetu havina nidhamu kwanza hawahudhurii vikao, pia wana matumizi mabaya ya fedha, wengine ni waheshimiwa lakini ni wezi, kuna mmoja siwezi kumtaja kwa jina nilimkamata na gari la wizi nikamwambia ashuke japokuwa ni mbunge, ninawaomba fedha za usajili zitumike vizuri si mzigombanie,” amesema.

Suala la tatu ambalo Dk. Bashiru amelizungumzia katika mdahalo huo ni utegemezi ambapo amesema vyama vingi havina vyanzo vya ndani hivyo kuvifanya kuwa tegemezi.

“Vyama vyote ni tegemezi haviendeshwi kwa vyanzo vya fedha zao wenyewe, wafukuzeni matajiri wanaoleta fedha kupanga safu za madaraka kwa kufanya hivyo tutakuwa tumejikomboa, bila vyama kuendeshwa na vyanzo vya ndani kuna hatari matajiri wakaingia na kutupangia nini cha kufanya,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles