24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Bashiru aagiza uchuguzi Sh mil 300

Ashura Kazinja,Morogoro

KATIBU Mkuu Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Loata Ole Sanare kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini gharama halisi iliyotumiwa na Kampuni ya Reli ya Mwendokasi (SGR) kwenye ujenzi wa kituo cha afya Mikese kutokana na  uwepo wa ubadhilifu wa Sh milioni 300.

Dk. Bashiru aliyasema hayo mwishoni mwa wiki mkoani hapa, wakati akiwa wa ziara yake ya siku tatu  kwa ajili kukagua utekelezaji wa ilani ya chama chake.

Akiwa kwenye mradi wa ujenzi wa kituo cha afya Mikese, ilibainika uwapo wa ujenzi wa jengo jingine la mapokezi linalojengwa kwa fedha za fidia ya SGR kufuatia kubomolewa kwa zahanati ya Mikese kupisha ujenzi wa reli ya mwendokasi ujenzi ambao haujalingana na thamani ya fedha iliyotolewa.

“Nimeenda pale Mikese, nikaambiwa kuna kituo kimejengwa kama fidia ya zahanati ambayo imepitiwa na mradi wa reli ya mwendo kasi, eti thamani yake shilingi milioni 300, kini majengo karibu saba yaliyoko pale yaliyojengwa na serikali kwa usimamizi wa halmashauri ni milioni 380, chumba kimoja nilichokiona pale eti milioni 300, pale kuna shida kwa nini wasingewakabidhi nyie hizo fedha mjenge,” alisema.

Alisema ni vyema uchunguzi ukafanyika ili kubaini kama kabla ya kuvunja zahanati hiyo walifanya tathmini na kufikia kutoa Sh milioni 300 kama fidia na kuhakikisha kama kuna ukweli kuwa walikubaliana wajenge wenyewe vyumba kwa gharama hiyo.

Sanare alisema ujenzi wa kituo cha afya mikese unaenda sambamba na ujenzi wa jengo moja la mapokezi linalogharimu kiasi kufidia kubomolewa kwa zahanati ya kijiji gharama ambayo itatumika pia kwa kuweka samani kwenye nyumba hiyo.

Aliwataka watendaji wa halmashauri kuhakikisha wanazingatia matumizi ya rasilimali za umma na kujiepusha na ubadhilifu ambapo ameahidi kuwachukulia hatua  watakapobainika.

“Suala la ubadhilifu halitafumbiwa macho, zipo fedha zililetwa kwa ajili ya kuwakomboa na kuwatendea haki wananchi wa Morogoro Vijijini, lakini fedha hizo Sh bilioni 1.5 zilizotolewa na Serikali na kilichofanyika hakionekani na mpaka sasa Sh milioni 500 haijulikani imeenda wapi,”alisema.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Rehema Bwasi alisema halmashauri inatekeleza miradi mbalimbali ambapo vituo 6 vya afya tayari vimejengwa na hospitali ya wilaya moja kuboreshwa kwa gharama ya Sh bilioni 4 zilizotolewa na Serikali.

Alisema jengo la mapokezi (OPD) la kituo cha afya Mikese, limejengwa na Kampuni ya  SGR na kugharimu Sh milioni 300.

Akiwa katika kikao cha ndani na viongozi wa CCM Wilaya ya Morogoro, Dk. Bashiru alisema huu ni mwaka wa uchaguzi na kuwaonya wanaoonekana kuvunja kanuni za uchaguzi kwa kubeba wagombea mifukoni kuacha mara moja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles