24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Bashe: kuna upotevu wa zaidi ya Bilioni 120 kwenye vyama vya ushirika

Derick Milton, Mwanza

Naibu Waziri wa kilimo Hussein Bashe amesema kwa mujibu wa ripoti ya ukaguzi ya shirika la Ukaguzi wa Vyama vya Ushirika (COASCO), wamebaini kuwepo kwa upotevu wa jumla ya shilingi Bilioni 123 kwenye vyama vya ushirika.

Ameyasema hayo leo wakati akifungua kikao cha wadau wa bodi ya pamba nchini kinachofanyikia kwenye ukumbi wa benki kuu (BOT) jijini Mwanza ambapo ameeleza kuwa wahusika wote watachukuliwa hatua kali.

“Hapa nina kabrasha, nitawapatia wakuu wa mikoa wote, na nitamkabidhi kiongozi wa tume, kwa ripoti ya COASCO ushirika kumetokea jumla ya upotevu wa sh. Bilioni 123, na nisema hapa hatua kali zitachukuliwa kwa wahusika wote,” amesema.

Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe akiongea na wajumbe wa kikao cha wadau wa pamba nchini.

“Hizi ni pesa za wakulima, wote waliohusika katika huu upotevu watachukuliwa hatua kali, na wakuu wa mikoa tutawapa majina ya Amcos gani wanahusika na mnatakiwa kuchukua hatua,” amesema Bashe.

Adha ameongeza kuwa ushirika uliopo kwa sasa unahitaji mabadiliko makubwa kwani hauwezi  kutatua matatizo ya kilimo hasa kwenye zao la pamba, ambapo mfumo unatakiwa kubadilishwa kutoka ushirika wa kuhudumia wakulima na kuwa ushirika wa kibiashara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles