30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

BARNABA AKAMILISHA NYIMBO 100

Na JENNIFER ULLEMBO


MSANII wa muziki wa Kizazi kipya, Barnaba Elias ‘Barnaba Classic’, amesema ataendelea kuachia wimbo baada ya wimbo, ili kuhakikisha anatoa burudani ya kutosha kwa mashabiki wake.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Barnaba alisema amekamilisha nyimbo zaidi ya 100, hivyo atakachofanya ni kushauriana na watayarishaji wake kuchagua wimbo wa kuingiza sokoni.

Alisema yeye ni msanii mkubwa anayetumia vema kipaji chake, ambapo mara nyingi amekuwa akitumia muda wake wa ziada kuandaa nyimbo mbalimbali ili kujiwekea akiba.

“Mimi ni msanii ninayetambua vema jinsi ya kutumia kipaji changu, muda ambao nimekuwa sina majukumu yanayonibana sana lazima utanikuta naandaa kazi zangu,” alisema Barnaba.

Msanii huyo kwa sasa anatamba na nyimbo zake mbili alizoziachia hivi karibuni, ambazo ni Tunafana pamoja na Mapenzi Jeneza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles