BARNABA AENDELEA KUMUWAZA FALLY IPUPA

0
201

Na JENNIFER ULLEMBO–DAR ES SALAAM


 

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Barnaba Elias ‘Barnaba Classic’, amesema bado ndoto zake za kufanya kazi ya pamoja na msanii, Fally Ipupa, kutoka nchini Congo zipo pale pale.

Akizungumza hivi karibuni, msanii huyo alisema mipango yake bado inaendelea kwani mbali ya kufanya kazi na msanii huyo, pia anahitaji kusaka wasanii wengine wakimataifa.

“Ndoto zangu za kufanya kazi na Fally Ipupa zipo palepale ni msanii ambaye nimekuwa nikivutiwa naye tangu nilipoanza kuwa mwanamuziki,” alisema Barnaba.

Barnaba alisema kwa sasa anaendelea na mipango yake ya kuachia albamu mpya, ambayo itakuwa na ‘surprise’ mbalimbali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here