28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Bares aanza kuipigia tizi Simba

Theresia Gasper -Dar es salaam

KIKOSI cha JKT Tanzania kimeanza mazoezi rasmi ya kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba, unaotarajiwa kuchezwa Agosti 29, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Timu hiyo ilijichimbia Zanzibar kwa kambi ya  wiki tatu,  kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya , kabla ya kurejea Dar es Salaam yaliko makao yake makuu Jumatatu wiki hii, ambapo wachezaji walipewa mapumziko ya siku nne ksiha jana kuingia kambini.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Abdallah Mohammed ‘Bares’, alisema wameanza kuipigia hesabu Simba, kwa kuangalia mechi zao ili kutafuta mbinu za kuikabili na kupata ushindi.

“Tumeanza kambi leo (jana), baada ya mapumziko mafupi, tunafanya mazoezi asubuhi kujiandaa na mchezo wetu wa kwanza wa Ligi Kuu dhidi ya Simba,” alisema.

Alisema kwa kuzingatia maandalizi wanayofanya, anaamini watauanza msimu mpya vizuri tofauti na ule uliopita.

“Lengo letu ni kuanza msimu kwa kuvuna pointi tatu, tumefanya mandalizi ya kutosha, tulikuwa Zanzibar kule tulipata wasaa mzuri wa kujiandaa.

“Kipindi hiki kifupi kilichobakia niendelea kutafutia ufumbuzi wa kasoro nilizoziona katika michezo yetu ya kirafiki kabla ya kukabiliana na Simba, naamini tutafanya vizuri,”alisema Bares.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles