27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Baraza lote la mawaziri lajiuzulu Mali

Rais Ibrahim Boubacar Keita wa Mali amekubali ombi la kujiuzulu kwa Waziri Mkuu na baraza lake zima la mawaziri.

Soumeylou Boubeye Maiga alichukuwa hatua hiyo hapo jana, kufuatia wiki mbili za maandamano ya umma dhidi ya mauaji ya kiholela katika taifa hilo la magharibi mwa Afrika.

 Maandamano hayo yalichochewa na mauaji ya wachungaji 160 wa jamii ya Fulani, ambayo yanashukiwa kufanywa na watu wa jamii ya Dogon, wanaoishi kwa kilimo na uwindaji.

Mauaji hayo yaliitikisa Mali, ambayo katika miezi ya karibuni imeshuhudia mauaji mengine kadhaa, yakiwemo yale ya wanajeshi 23 walioshambuliwa kwenye kituo chao.

Juzi Jumatano, bunge lilijadili uwezakano wa kura ya kutokuwa na imani na serikali kutokana na mauaji hayo na pia kushindwa kuwanyang’anya silaha na kuwazuwia wanamgambo wa itikadi kali.

Umoja wa Mataifa una zaidi ya wanajeshi 16,000 nchini Mali, vikiwemo vikosi kutoka Ufaransa na Ujerumani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles