27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Bandari ya Musoma yaanza kwa kasi

Mwandishi Wetu, Musoma

Bandari ya Musoma imeanza kazi kwa kasi baada ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kuimarisha ujenzi wa gati moja na ghala la mizigo katika ikiwamo kupokea na kuhifadhi mizigo huku idadi ya meli zinazoingia ikiongezeka.

Akizungumza mjini Musoma mkoani Mara, leo Ijumaa Desemba 6, Meneja wa Bandari za Ziwa Victoria, Morris Machindiuza amesema licha ya ukarabati huo wa miundombinu bandarini hapo, kwa sasa wako mbioni kufufua daraja linalounganisha kati ya meli na reli ambapo ujenzi wake utaanza Januari na kukamilika Aprili 2020 huku ukitarajiwa kutumia Sh milioni 650 ambazo ni fedha za ndani.

“Hii Bandari ya Musoma ilianza kujenga mwaka 1966 na kukamilika mwaka 1968 lakini kwa miaka 10 iliyopita ilishindwa kufanya kazi kutokana na kile tunaweza kusema mdororo wa uchumi.

“Hata hivyo kwa sasa tumekuwa tukitafuta masoko mapya na sasa tayari kuna mteja mmoja ameanza kutumia kwa kupakia na kushusha mizigo yake na Januari 2020 wateja wengine wawili nao wameomba kuanza shughuli zao.

“Bandari za Ziwa Victoria tumeziimariaha zote na mkakati wetu ni kuhudumia nchi zote za Afrika Mashariki. Ingawa kwa sasa tumesafirisha shehena ya mzigo katika nchi za Sudan Kusini, Uganda, Rwanda na Kenya ambapo tumeanza kusafirisha mashudu kuelekea Bandari ya Kisumu,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles