23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

BANDA: SIMBA KUTWAA UBINGWA VPL NDOTO

NA SAADA SALIM- ZANZIBAR

BEKI wa Baroka FC ya Afrika Kusini, Mtanzania Abdi Banda, anaamini Simba imejimaliza yenyewe katika vita ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) msimu huu, baada ya kumtimua aliyekuwa kocha wake, Joseph Omog.

Simba ilimfungashia virago Omog  mwishoni mwa mwaka jana, ikiwa ni siku moja baada ya timu hiyo kushindwa kutetea ubingwa wake wa Kombe la Shirikisho la Azam ilipoondolewa katika hatua ya 64 bora kwa kuchapwa penalti 4-3 na timu ya daraja la pili ya Green Warriors.

Akizungumza na MTANZANIA, Banda, aliyejiunga na Baroka akitokea Simba, alisema hatua ya kumfuta kazi Omog imeondoa uwezekano wa timu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

“Mimi nimeshangaa sana, ukiwa hapa Afrika Kusini makocha wanaosifika ni Omog na Hans Pluijm, lakini Simba wamemfukuza kwa sababu ambazo  hazina maana.

“Haya ni matokeo ya kuwa na viongozi wasio na uchungu na timu zaidi ya masilahi yao, nakwambia walichokifanya kitaigharimu Simba na pengine mambo ya ubingwa yakabakia kuwa ndoto,” alisema Banda.

“Hapa kuna suala la viongozi kuangalia asilimia 10 katika mchakato wa kumleta kocha mpya, ni jambo lisiloingia akilini.”

Akizungumzia hatua ya Simba kufanya vibaya katika michuano ya Mapinduzi ilipoondolewa katika hatua ya makundi, alisema anaamini kumetokana na viongozi  kuingilia majukumu ya benchi la ufundi.

“Mfumo wa 3:5:2 tuliwahi kutumia wakati tunafundishwa na Dylan Kerry, lakini inategemea na timu unayokutana nayo.

“Hatukuwa tunatumia mfumo huu tunapocheza na Azam FC au Yanga, alikuwa akibadilisha kulingana na aina ya mpinzani tunayekutana naye,” alisema Banda.

Alisema kama Kocha Masoud Djuma, ataendelea kutumia mfumo huo, kuna hatari Simba itakapokutana na timu yenye njaa ya mabao itaambulia kipigo cha aibu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles