Imechapishwa: Fri, May 18th, 2018

BADO MIAKA MITANO DAVIDO KUACHA MUZIKI

LAGOS, NIGERIA


NYOTA wa muziki nchini Nigeria, David Adeleke ‘Davido’, ametangaza kuwa amebakisha miaka mitano kuachana na maisha ya muziki.

Msanii huyo ambaye ametajwa kuwania tuzo ya Black Entertainment Television (BET), nchini Marekani mwaka huu, amedai kuwa hana muda mrefu wa kuendelea kufanya muziki.

“Kwa sasa nina umri wa miaka 25, mipango yangu kwa sasa ni kuhakikisha ninaitumia miaka mitano iliyobaki ili kutimiza 30 niweze kuachana na maisha ya muziki, baada ya hapo sitakuwa na mpango wa kuendelea kufanya muziki kwa ubora wangu na ndio maana ninataka kuachana nao,” alisema Davido.

Katika tuzo hizo za BET, Nigeria wamefanikiwa kutoa wasanii wawili kuwania tuzo hizo katika kinyang’anyiro cha msanii bora wa kutumbuiza, hivyo Davido ametajwa kuungana na Tiwa Savage.

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

YOUTUBE

BADO MIAKA MITANO DAVIDO KUACHA MUZIKI