30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

BADILI MTAZAMO, UBADILI MWELEKEO WA MAENDELEO

 

 

NA DK. SHRIS MAUKI,

TOFAUTI kubwa kati ya maeneo ya biashara, ujasiriamali, kazi za kuajiriwa au vitu vingine vyovyote kama vile; matumizi ya barabara, maisha ya familia n.k. ni katika maadili ya maeneo hayo. Ni karibu ya asilimia 5 hadi 10 tu ya watu walioko katika kazi zao za kitaalamu au zisizo za kitaalamu ambao wanafuata maadili ya kazi (Work Ethics), wengi tunakwenda kwa mazoea, tunafuata hali tuliyoikuta na kuiendeleza pasipo kujiuliza kama hali hiyo inajenga au kudumaza taaluma. Matokeo yake siku zote tumekuwa tukilia maendeleo ambayo hatuyaoni na wala hatutayaona na hata kama yatakuja basi kwa kuchelewa sana.

Sisi kama mashahidi tujiulize, je, hutujawahi kuona mfanyakazi kusoma gazeti au magazeti ofisini wakati kuna majukumu yanamsubiri kufanya? Na wala hasiishie tu kwenye kusoma gazeti bali hata kwenye kuyajadili yote wanayoyasoma, iwe watu, habari, picha, nyimbo, katuni hadi matangazo ya biashara yatajadiliwa. Sasa hapa simaanishi magazeti ni mabaya, bali ubaya unabaki akilini mwa huyo mfanyakazi asiyeweza kupangilia kuwa saa ngapi asome gazeti na saa ngapi afanye kazi zake, mbaya zaidi mwingine anafanya hivi kwenye sehemu yake ya kujiariri akisahau ule usemi usemao ‘Time is money’ wakati ni pesa, halafu mtu huyu huyu anashinda akilalama maisha magumu, hela ngumu, wakati hela anaimwaga nje kila kukicha anapoteza muda.

 Je, hujawahi kuona wafanyakazi wakiweka vikao visivyo rasmi kuongelea habari za nje ya ofisi muda wa ofisini? Kwa bahati mbaya mazungumzo haya huonekana kuwa matamu sana na yanayochukua mwelekeo mzuri na unaovutia, taratibu ya kila muda mrefu wa wafanyakazi hawa pasipokugundua athari zake. Lakini watu hawa hawa nirahisi kulalama kuongezewa mshahara mwisho wa mwezi na mara wanapoambiwa kampuni au ofisi haijapata faida, huwa wakali sana na ukweli ni kwamba wamejinyima mishahara mikubwa wenyewe. Je haujawahi kuona? Wafanyakazi au hata mfanyabiashara fulani kama duka au biashara yeyote akienda kula kwa zaidi ya lisaa limoja? Mara ngapi tunaenda kwenye mabenki au ofisi ambazo huduma hutolewa kwa kupanga foleni, inapofika saa sita na nusu kama watoa huduma walikuwa watano anabaki mmoja na foleni zote zinahamia kwa mtu huyu mmoja kwa muda mrefu tu. 

Wengi wetu tukifika tu ofisini asubuhi raha na mawazo yetu hayaelekezwi katika utendaji wa siku hiyo bali katika kuutazamia kwa hamu muda wa kutoka kwenda kula, utasikia mtu akijibu simu akisema: “Subiri nitakupigia tuongee vizuri muda wa kula,” “Unaonaje tukionana muda wa kula,” “Basi pita hapa mida ya lunch mchana?” “Ntachomoka kidogo nije wakati wa chakula cha mchana.” Mazungumzo haya yote yanamwandaa mfanyakazi huyu kisaikolojia kuhifadhi nishati kubwa ya kutumika wakati wa kupumzika kwenda kula zaidi ya nishati hiyo ya mwili kutumika wakati wa kazi kwa manufaa ya ofisi au kampuni.   

Je umewahi kuona mfanyakazi kuwapa kipaumbele wale unaowajua au wenye manufaa kwake kwa namna   fulani? Labda waliwahi kuwa pamoja shuleni au chuoni, labda wanatoka wote kijiji au mkoa mmoja na lugha yao ni moja, labda wazazi au wazee wao ni marafiki, labda ni ndugu wa upande wa mama au baba au wakwe, au labda ni mtu wa kike au wa kiume ambaye moyo wako umewahi kumfikiri zaidi kihisia. Katika hali zote hizi ukasahau kwamba kama ilivyo katika sheria kwamba kila binadamu ana haki sawa mbele ya sheria ndivyo hivyo hivyo  katika maadili ya kazi kila mteja ana haki sawa kihuduma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles