Imechapishwa: Sun, Nov 27th, 2016

Babu wa miaka 86 jela kwa kumbaka bintiye wa miaka 8

hands_on_prison_bars

Na MURUGWA THOMAS – TABORA

MZEE Nassoro Mbavumbili (86), mkazi wa Wilaya ya Urambo mkoani Tabora, amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kufanya mapenzi na binti yake.

Adhabu hiyo imetolewa juzi na  Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Urambo, Hassan Momba, baada ya babu huyo kutiwa hatiani kwa kufanya mapenzi na binti yake huyo (jina linahifadhiwa) mwenye umri wa miaka minane.

“Kwa kuzingatia ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka, mahakama hii imethibitisha pasipo kuacha shaka kwamba mshtakiwa Mbavumbili alitenda kosa la kufanya mapenzi na binti yake wa kumzaa mwenye umri wa miaka minane kwa makusudi,” alisema Momba.

Mshtakiwa Mbavumbili anadaiwa kutenda kosa hilo kati ya mwezi Januari na Oktoba 20, mwaka huu kinyume na kifungu namba 158 (1) (a) cha makosa ya jinai.

Awali  upande wa mashtaka  ukiongozwa na Mkaguzi wa Polisi,  Phillibert  Pimma,  uliieleza mahakama hiyo kuwa  kati ya Januari na  Oktoba 20, mwaka huu katika  tarehe tofauti tofauti, mshtakiwa Mbavumbili alikuwa akifanya mapenzi  na binti yake  huyo.

Alisema Mbavumbili   amekuwa akifanya kitendo hicho huku akimtishia mtoto huyo kutosema kwa mtu yeyote na endapo angekiuka angeweza kumdhuru uhai wake.

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

FACEBOOK

YOUTUBE

Translate »

Babu wa miaka 86 jela kwa kumbaka bintiye wa miaka 8