33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Azam yaleta kipa Mhispania

NA THERESIA GASPER, DAR ES SALAAM

KLABU ya Azam FC juzi ilimleta kipa raia wa Hispania, Juan Jesus Gonzalez, kufanya majaribio ya kujiunga na timu hiyo katika msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Ujio wa kipa huyo unatokana na matakwa ya benchi jipya la ufundi la Azam FC chini ya kocha,  Zeben Hernandez, ambalo linataka kuongeza nguvu langoni na kutengeneza safu bora ya ulinzi na ushindani wa namba katika nafasi hiyo.

Gonzalez ambaye ni mrefu wa kutosha, aliwasili nchini juzi na alipokelewa na Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffar Idd, ambapo ataanza rasmi majaribio yake mara baada ya kikosi cha Azam FC kuanza mazoezi ya maandalizi ya msimu mpya.

Kwa mujibu wa mtandao wao, kocha Zeben aliona eneo hilo ni sehemu muhimu sana ambalo alipanga kuliongezea nguvu zaidi.

“Nimefurahi sana kufanikiwa kwake kutua hapa, namjua Gonzalez ni kipa mzuri na hili ni jambo muhimu sana kwa Azam FC katika kuboresha eneo hilo, atakuwa hapa kwa majaribio akifanya vizuri tutamchukua,” alisema.

Hii ni mara ya pili kwa Azam FC kumleta kipa Mzungu ndani ya kikosi chake, mwaka 2011 iliwahi kumnasa kipa kutoka nchini Serbia, Obren Cirkovic, ambaye alianza kuwika akiwa na timu ya Yanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles