28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Azam yaiwinda Bidvest Wits

KITAMBI-1NA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM

TIMU ya soka ya Azam imeanza kujiwinda kuelekea kwenye michuano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho kwa kuanza kuwasoma wapinzani wao wanaotarajia kukutana nao katika raundi ya kwanza ya michuano hiyo.

Azam waliopita moja kwa moja katika raundi hiyo bila kucheza hatua ya awali, Jumamosi iliyopita ilituma makocha wao wasaidizi Mario Marinica na Dennis Kitambi, kwenda nchini Shelisheli kushuhudia mchezo wa raundi ya awali ya michuano hiyo uliowakutanisha wenyeji Light Stars na Bidvest Wits ya Afrika Kusini, ambapo mwisho wa mchezo wageni walishinda mabao 3-0.

Akizungumza na MTANZANIA, Kitambi alisema walikwenda kuwaona wapinzani hao kujua udhaifu na uzuri wao ili wasipate tabu watakapokutana nao.

“Kutokana na matokeo hayo ya ushindi kwa Bidvest Wits, ni wazi tutakutana na timu hiyo tumegundua wapinzani wetu wana kikosi cha wachezaji wengi vijana, lakini waliwatumia katika mchezo dhidi ya Light Stars ili kuwapumzisha wachezaji wa kikosi cha kwanza wakongwe, tunajua ni wachezaji wa aina gani watapangwa siku hiyo,” alisema Kitambi.

Kitambi alisema mwanzo walishawasoma Bidvest kupitia michezo yao ya Ligi Kuu Afrika Kusini, lakini walishangaa timu hiyo ilivyobadilika na kuanza kutumia kikosi cha vijana zaidi kuliko walivyotarajia.

Hata hivyo, alieleza wanajiandaa kusafiri kuelekea Afrika Kusini kuwasoma tena Bidvest Wits, katika moja ya mechi yao ya ligi ili kuwaelewa zaidi wapinzani wao hao wanaofundishwa na kocha Gavin Hunt.

Alisema maandalizi ya michuano hiyo yanaendelea vizuri, akieleza kuendelea kushiriki michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara itawajenga na kuwafanya kuwa na kiwango kizuri zaidi.

“Michezo miwili ya ligi tutakayocheza kabla ya kukutana na wapinzani wetu kwenye michuano ya Shirikisho Afrika, itatusaidia hivyo hakuna wasiwasi juu  ya kiwango chetu licha ya hivi karibuni kufungwa na timu ya Coastal Union ya Tanga,” alisema Kitambi.

Timu ya Azam kwenye michuano hiyo inatarajiwa kuchanga karata zake ugenini kwa kucheza mchezo wake wa kwanza  dhidi ya timu ya Bidvest Wits kati ya Machi 11, 12 na 13 kabla ya kumalizia nyumbani kati ya Machi 18,19 na 20.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles