23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

AVEVA, KABURU WATUPIA LAWAMA MAWAKILI KUCHELEWESHWA KESI YAO

PATRICIA KIMELEMETA


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa siku saba kwa upande wa Jamhuri kukamilisha mchakato wa kubadilisha hati ya mashtaka ili kuwaondoa washtakiwa wawili katika kesi inayomkabili aliyekua Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva na makamu wake, Godfrey Nyange (Kaburu).

Washtakiwa wanaotakiwa kuondolewa katika kesi hiyo ni Zacharia Hanspope na Frank Lauwo ambao hawajawahi kufika mahakamani hapo.

Awali, wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai aliieleza mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa.

Alidai tayari wameshaifanyia marekebisho hati ya mashtaka na kwamba wanasubiri kibali cha mkurugenzi wa mashtaka (DPP) ili kesi hiyo iweze kuendelea kwa mujibu wa sheria.

Mara baada ya kudai hayo, mshtakiwa wa kwanza, Aveva aliiomba mahakama hiyo kupanga tarehe za karibu ili waweze kusikiliza kesi hiyo kwa madai kuwa imechukua muda mrefu huku wakili wa Jamhuri, Shadrack Kimaro na wa Takukuru, Swai wamekuwa wakirushiana mpira.

Mshtakiwa wa pili, Kaburu amedai kuwa ni zaidi ya mwaka mmoja sasa umepita wapo mahabusu tangu kesi hiyo ianze kusikilizwa mahakamani hapo huku mawakili hao wakidai faili lipo kwa DPP.

Alidai mshtakiwa wa kwanza, Aveva ana matatizo ya kiafya na kwamba kila wiki anaenda kliniki kwa ajili ya matibabu hivyo kuendelea kurushiana mpira ni kuwaumiza.

Alidai hadhani kwamba si DPP ameshindwa kushughulikia kesi yao, bali ni ucheweshaji wa makusudi unaofanywa na mawakili hao katika kesi hiyo kutoka kwa DPP na Takukuru.

Alidai upelelezi umeshakamilika kilichobaki ni kubadilisha hati hiyo ili kesi ianze kusikilizwa, hivyo aliiomba mahakama hiyo kupanga tarehe za karibuni ili waweze kuwaona na kuwaonea huruma kuliko kupanga tarehe za mbali.

Wakili Swai alidai kuwa hoja zilizotolewa na washtakiwa hao zina mashiko na kuahidi kushughulikia suala hilo.

Hata hivyo, Hakimu Simba alitoa siku saba kwa upande wa Jamhuri kukamilisha mchakato wa kubadilisha hati ya mashtaka ili kesi hiyo iweze kusikilizwa.

“Ukiangalia afya ya Aveva unaona kabisa ni mgonjwa, anatakiwa kwenda kliniki kwa wiki mara mbili, hivyo basi tunalazimika kuangalia ratiba ya matibabu yake ili tupange kesi,” alisema Hakimu Simba.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles