27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Aussems hana uhakika wa kuwapo Simba msimu ujao

Tima Sikilo, Dar es Salaam

Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, amesema kufanya usajili kwenye kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao itategemea kama ataendelea kuwepo kwenye kikosi hicho.

Aussems alisajiliwa mwanzoni mwa msimu huu 2018/19, kwa mkataba wa mwaka mmoja akichukua nafasi ya Mfaransa, Pierre Lechantre hivyo mkataba huo unatarajia kumalizika mara baada ya msimu huu kuisha.

Akizungumza na Mtanzania Digital, leo Aprili 5, Aussems amesema iwapo kama angekuwa na uhakika wa kuwepo msimu ujao wa 2019/20 angejua afanye usajili wa aina gani.

“Mkataba wangu upo mwishoni hivyo siwezi kutaja mchezaji ninayetaka kumsajili wakati sijui kama msimu unaofuata nitaendelea kuwa mwongozaji wa gurudumu la kikosi cha Simba ,” amesema Aussems.

Aidha, kocha huyo ameweka wazi kuwa tetesi zilizopo kuhusu Meddie Kagere na Jonas Mkude kutakiwa na timu nyingine ni habari ambazo anazisikia lakini hafahamu chochote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles