23 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

ATRC YAGUNDUA DAWA MPYA ZA KUUA MBU

Na ELIYA MBONEA-ARUSHA

TAASISI ya Utafiti wa Wadudu na Mazao Afrika (ATRC), imegundua dawa mbili mpya za kuua mbu na mazalia yake katika harakati za kupambana na ugonjwa wa malaria.

 

Uzinduzi wa dawa hizo ulifanyika juzi katika hafla fupi ambapo taasisi hiyo iko chini ya kiwanda cha kutengeneza chandarua na nguo cha A to Z, ulioenda sambamba na maadhimisho ya miaka mitano tangu kuanzishwa kwake.

 

Balozi wa Japan nchini, Masaharn Yoshida, alisema ugunduzi wa dawa hizo mpya SumiShield na SumiLove ni suluhisho la ugonjwa wa malaria ambao umekuwa tishio kwa ukanda wa Afrika ikiwamo Tanzania.

 

Alisema kituo hicho ambacho kinamilikiwa kwa ubia kati ya Kampuni ya Sumitomo ya Japan na A to Z ya Tanzania, kimekuwa kikifanya kazi nzuri ya kuhakikisha inasaidia kutafiti viuatilifu ambavyo vitasaidia kupambana na magonjwa pamoja na wadudu waharibifu katika mazao.

 

“Serikali ya Japan itaendelea kuisaidia Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo hiyo ya utafiti ili kuhakikisha magonjwa hatarishi yanakabiliwa pamoja na mapambano dhidi ya wadudu waharibifu wa mazao,” alisema Balozi huyo.

 

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa A to Z , Kalpesh Shah, alisema kituo hicho kilichoanzishwa mwaka 2012, kimekuwa chachu kubwa ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria kwa kuzuia vifo vya akina mama na watoto kwa kutengeneza vyandarua.

 

Shah alisema kupitia kituo hicho cha utafiti wa wadudu na mazao Afrika, A to Z vitaendelea kusaidia Watanzania na Afrika kwa ujumla katika kutafiti viuatilifu mbalimbali kwa ajili ya kupambana na maradhi ambayo yamekuwa yakisababisha vifo vya watu wengi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles