25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

ASKOFU SHOO ATAMANI WATANZANIA KUVAA UJASIRI KUKEMEA UOVU

Na Upendo Mosha, Moshi

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk.  Fredrick Shoo, amesema anatamani kuona Wakristo na Watanzania wote wanavaa ujasiri na kuwa na sauti ya kuonya  kwa kusema watu wamuogope Mungu kwa maovu yanayofanyika .

Dk. Shoo ambaye pia ni Askofu wa KKKT Dayosisi ya kaskazini, ameyasema hayo leo Jumapili Aprili 8, wakati akiongoza ibada katika Usharika wa Msaranga, mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

Amesema katika dunia hii iliyojaa watu wenye midomo michafu, waliojaa viburi na unafiki mkubwa ambao hawaoni madhaifu yao ni vema Watanzania na Wakristo wakaungana katika kutoa maonyo dhidi ya watu hao kwa lengo la kuwafanya watu wote waishi kwa amani bila hofu.

“Katika dunia hii iliyojaa watu wa aina hiyo wenye kukata tama, wanaokataa maonyo, wasioona madhaifu yao na wanaokataa kutubu, Yesu anasema nimtume nani awapelekee ujumbe, kwa mantiki hiyo natamani kuona Wakristo watakatekeleza haya bila hofu.

“Kanisa linatamani kuona Watanzania wanaishi katika hali ya amani, upendo, mshikamano, maelewano pasipo kujali vyeo vyao wala  itikadi zao za  kisiana na ubaguzi wa kikabila na ukanda,” amesema.

Dk. Shoo amesema kumekuwa na watu wanaojinadi kwa maneno mazuri katika kuhubiri amani na mshikamano jambo ambalo halina uhalisia na kwamba Wakristo na Watanzania wana wajibu wa kusimama na kuhubiri amani na mshikamono wa kweli kwa vitendo.

“Katika nchi yetu kumekuwa na watu wanaojua kuyapamba maneno kweli kweli kisha wanasema wanahubiri amani ya Yesu mfufuka lakini maisha na mienendo yao iko kinyume kabisa na hilo hivyo wakati umefika Wakristo tuhubiri haki ya kweli, upendo na mshikamano,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles