23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Asilimia 96 ya wazawa waajiriwa mradi wa SGR, wageni asilimia nne

Nora Damian, Dar es Salaam




Zaidi ya watu 6,000 wameajiriwa katika mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR).

Kati ya ajira hizo asilimia 96 sawa na watu 6,182 ni za Watanzania na asilimia nne sawa na watu 258 ni wageni.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Jumanne Novemba 14, kuhusu maendeleo ya mradi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa, amesema kwa upande wa wataalamu 189 ni Watanzania na 258 ni wageni.

“Ajira 626 za Watanzania wasio na ujuzi na 19 za wenye ujuzi zimepatikana kupitia kampuni za wazawa wanaoshiriki moja kwa moja kwenye mradi huu, hivyo tunafanya vizuri sana,” amesema Kadogosa.

Amesema maendeleo ya ujenzi huo kwa kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro yamefikia asilimia 34.

Kipande hicho chenye urefu wa kilomita 300 kilianza kujengwa Mei 2, mwaka jana na kinatarajiwa kukamilika Novemba 2, mwakani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles