31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Asilimia 24 ya watoto njiti miili yao haina kinga

Na  AVELINE  KITOMARY-DAR ES SALAAM

DAKTARI bingwa wa magonjwa ya watoto wachanga kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk.Augustine Massawe amesema asilimia 24 ya vifo vya watoto wachanga vinatokana na watoto wanaozaliwa njiti kwa sababu miili yao haina kinga. 

Akizungumza na katika mahojiano maalumu  MTANZANIA Dar es Salaam jana, Dk. Massawe alisema sababu za watoto kuzaliwa njiti, ni  lishe duni na magonjwa kwa wajawazito, imekuwa ikichangia ongezeko la watoto wanaozaliwa njiti.

“Tanzania pekee kuna  watoto milioni 2  wanaozaliwa kati ya watoto 10, moja ni njiti kwa hiyo wanaozaliwa njiti sio chini ya 250,000 kwa mwaka.

“Vifo vingi vya watoto walioko chini ya mwezi mmoja,Tanzania ni hivyo watoto wanaozaliwa njiti kutokana hawana kinga ya mwili unakuwa na matatizo ya kuhimili ‘temperature’ ,mapafu kutokukomaa hata kumlisha huwezi, mama anakaa hospitali muda mrefu,”alisema .

Alisema sababu zingine ni umri mdogo wa mama au mama mwenye umri mkubwa  wako hatarini kuzaa watoto njiti. 

“Lishe  duni ya mama ni hatari ya kuzaa njiti,nyingine magonjwa kama  upungufu wa damu kama anemia hii inaweza kusababisha mtoto kutoka mapema,kufanya kazi muda mrefu na ngumu hii pia inachangia.

“Asilimia 60 ya wajawazito wana upungufu wa damu, tatizo ni kubwa  na bahati mbaya wanaenda kliniki wamechelewa  hawaendi mapema ili kukorect anemia hilo ni tatizo moja, nyingine presha kupanda,kifafa cha mimba ,maambukizi ya magonjwa kama kifua au UTI au malaria hii inajulikana sana duniani  hapa mama anashindwa kutoa chakula kwa mtoto kingine ni ugonjwa wa kisukari,”alisema.

Aliwashauri kina mama kuzingatia lishe bora ,kufanya mazoezi na kupugunguza kazi ngumu pindi wanapokuwa wajawazito.

“Wakinamama wazingatie lishe bora anapobeba mimba awe tayari ana afya nzuri, awahi kliniki  na kujifungulia sehemu ambapo mtoto atahudumiwa vizuri, hii itasaidia kupunguza vifi vya watoto wachanga,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles