Asha Baraka atoa sababu za kuahirisha tamasha

0
1126

Na THEREZIA KIBAJA (TUDARCo)

MkurugenziI wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’, Asha Baraka, ameeleza sababu za kuahirishwa kwa tamasha la miaka 20 ya bendi hiyo.

Wiki chache zilizopita, bendi hiyo ilitarajiwa kuwapa burudani mashabiki wake katika kuadhimisha miaka 20, lakini ilishindikana na kuwaacha mashabiki njiapanda.

Asha amesema tamasha hilo bado lipo kwenye mipango na litafanyika rasmi Oktoba 27, mwaka huu katika ukumbi wa New Life Club.

“Napenda kuwajulisha wapenzi na mashabiki wetu wakubwa kwamba, tamasha la miaka 20 litafanyika Oktoba 27, katika ukumbi wa New life Club na wote mnakaribishwa, tulishindwa kufanya kama tulivyopanga kutokana na msiba mkubwa uliotokea katika ajali ya kivuko cha Mv. Nyerere,” alisema Asha.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here