ARUSHA UNITED YAENDELEA NA MECHI ZA KUJIPIMA NGUVU DAR NA PWANI

0
473

Msemaji wa Arusha United, Jamila Omari

Na ELIYA MBONEA, ARUSHA


LICHA ya timu ya Arusha United (Wana Utalii) kufungwa bao 1-0 na Namongo FC katika mchezo wa kirafiki, msemaji wa timu hiyo, Jamila Omar ameibuka na kusema mchezo huo umekiweka kikosi chao katika nafasi nzuri na ya kutia moyo katika safari yao ya mpira.

Jamila ameiambia Mtanzania Digital kwamba bao moja walilofugwa na timu hiyo ya daraja la kwana kwenye uwanja wa Halmashauri ya Namongo mkoani Lindi msimu huu limehamsha hali mpya kwa kikosi chao.

“Arusha United  tunaendelea  na maandalizi ya mashindano ya ligi daraja la kwanza msimu huu, tulipofungwa na Namongo wachezaji wote wameonekana kuwa na hali ya kutaka kucheza michezo mingi zaidia ili kujiweka sawa na michezo ya ligi daraja la kwanza. Na leo tunatarajia kucheza  mechi nyingine ya kirafiki katika Uwanja wa TAMCO mkoani Pwani na timu ya Kiluvya United,” alieleza Jamila.

Jamila amesema mechi nyingine ya kirafiki itapigwa kesho dhidi ya Adam Fc katika Uwanja wa Azam Complex na kabla ya kurejea Arusha kesho kutwa timu hiyo inatarajia kucheza na timu ya Friends Rangers katika Uwanja wa Kinesi jijini Dar es salaam.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here