24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Arsene Wenger aikataa timu ya taifa England

KOCHA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger
KOCHA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger

LONDON, ENGLAND

KOCHA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger, ameweka wazi kuwa hana mpango wa kutaka kuifundisha timu ya taifa ya England (Three Lions), akichukua nafasi ya Sam Allardyce, ambaye amefungashiwa virago.

Chama cha Soka nchini England (FA), kwa sasa kinahangaika kutafuta kocha ambaye atachukua nafasi ya Sam, lakini inadaiwa kwamba katika makocha ambao wametajwa kuwaniwa na chama hicho ni pamoja na jina la Wenger.

Hata hivyo, kocha huyo ambaye alikuwa anasherehekea miaka 20 ya kuitumikia klabu hiyo, amedai kwamba kwa sasa hana mpango wa kuondoka Emirates hadi pale mkataba wake utakapomalizika.

Mkataba wa kocha huyo unatarajia kumalizika mwishoni mwa msimu huu, hivyo hata kama England imelitaja jina lake hawezi kuachana na Arsenal kwa kipindi hiki.

Klabu hiyo juzi ilishuka dimbani katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya makundi na kufanikiwa kushinda mabao 2-0 dhidi ya FC Basel.

“Ni jambo la kushangaza kwa kile kilichotokea kwa Sam ambaye alikuwa anaifundisha England, hakuna ambaye alikuwa anajua nini kingeweza kutokea kwa kocha huyo kwa saa 48, lakini soka la nchini England siku zote ndivyo lilivyo.

“Inawezekana kuwa chama cha soka nchini England wananihitaji, lakini kwa sasa kitu ambacho ninakiangalia ni kuitumikia timu hii hadi mwishoni mwa msimu huu.

“Siku zote nimekuwa nikisema kuwa akili yangu ipo katika soka la klabu ya Arsenal, nitafanya hivyo hadi pale mwisho wangu wa kuitumikia timu hii, hivyo siwezi kufanya lolote kwa sasa,” alisema Wenger.

Nafasi ya Sam kwa sasa katika kikosi hicho cha England, imechukuliwa na aliyekuwa kocha wa timu ya vijana chini ya miaka 21, Gareth Southgate.

Wenger amewapongeza wachezaji wake katika mchezo wa juzi wa Ligi ya Mabingwa kutokana na ushindi walioupata wa mabao 2-0, huku yakiwekwa wavuni na mshambuliaji wao wa pembeni, Theo Walcott.

“Nitumie nafasi hii kuwapongeza wachezaji wote wa Arsenal kwa ushirikiano walioufanya na kufanikiwa kushinda dhidi ya Basel. Katika dakika 45 za mwanzo wachezaji walionesha uwezo wa hali ya juu na tulistahili kupata ushindi.

Michezo mingine ambayo ilipigwa juzi ni pamoja na PSG ambao walishinda mabao 3-1 dhidi ya Ludogorets Razgrad ya nchini Bulgaria, Besiktas ilitoka sare 1-1 dhidi ya Dynamo Kyiv, huku SSC Napoli ikiibuka na ushindi wa 4-2 dhidi ya Benfica.

Barcelona ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Borussia Moenchengladbach, Celtic ilitoka sare ya 3-3 dhidi ya Manchester City, Atletico Madrid ilishinda 1-0 dhidi ya Bayern Munich huku FC Rostov ilitoka sare ya 2-2 dhidi ya PSV Eindhoven.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles