Arsenal wamkumbuka Arsene Wenger

0
1532

LONDON, ENGLAND

ALIYEKUWA beki wa kati wa klabu ya Arsenal, Per Mertesacker, amefunguka na kusema, wachezaji walichangia kumwangusha aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Arsenal Wenger, bila ya kujali ya kuwa mtetezi wao.

Mertesacker amedai anajisikia vibaya kuwa miongoni mwa wachezaji ambao walishindwa kumpigania kocha huyo aendelee kuwepo, lakini aliungana na wachezaji hao kusababisha kocha huyo kufukuzwa.

Wenger alifukuzwa mwishoni mwa msimu uliopita mara baada ya kuwa hapo kwa kipindi cha miaka 22, lakini uongozi ulidai kuwa, umefikia hatua ya kuachana na kocha huyo kutokana na kushindwa kutwaa mataji katika kipindi cha hivi karibuni.

Mertesacker alisema Wenger alikuwa sahihi kuondoka kwa wakati huo, lakini wachezaji walisababisha kwa kiasi kikubwa.

“Kilikuwa kipindi kigumu sana, ambapo Wenger alikuja kutuambia kuwa anaondoka, kwa kuwa nilikuwa na hisia kali, huku nikiamini nimekuwa mmoja wa wachezaji ambao wamechangia kuondoka kwake.

“Wachezaji tulikuwa na kila sababu ya kupata matokeo mazuri, lakini tulishindwa kufanya hivyo na hatimaye kumsababishia kocha huyo matatizo, mara zote alikuwa pamoja na sisi katika kupigania haki zetu, lakini sisi tulishindwa kumpigania.

“Ukweli ni kwamba nitaendelea kujilaumu katika maisha yangu, lakini ndiyo maisha ya soka yalivyo,” alisema beki huyo wa zamani.

Mertesacker kwa sasa amepewa jukumu la kuwa kocha wa timu ya vijana ya Arsenal baada ya kuwa mchezaji wa klabu hiyo kwa miaka saba. Amecheza jumla ya michezo 156 ya Ligi Kuu na kufanikiwa kupachika mabao sita.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here