24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Arsenal, Chelsea zafanya kweli England

LONDON, ENGLAN



KIVUMBI cha michuano ya Ligi Kuu nchini England, kiliendelea jana kwa michezo mitatu kupigwa kwenye viwanja tofauti huku mchezo wa mapema ukiwakutanisha Chelsea ambao waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Fulham, huku Arsenal wakishinda mabao 4-2.

Moja kati ya michezo ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu ni ‘London Derby’ ambapo Arsenal walikuwa kwenye uwanja wa nyumbani dhidi ya wapinzani hao Tottenham.

Mchezo ulikuwa na ushindani wa hali ya juu huku kila timu ikifanya mashambulizi ya zamu kwa zamu, lakini Arsenal walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 10 ambalo lilifungwa na Pierre Aubameyang kwa mkwaju wa penalti baada ya beki wa Tottenham, Jan Vertonghen kuushika mpira kwenye eneo la hatari.

Hata hivyo Tottenham hawakukata tamaa walionekana kuopambana na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha katika dakika ya 30, likiwekwa wavuni na beki wao Eric Dier kwa kichwa kutokana na mpira wa adhabu uliopigwa na Christian Eriksen.

Baada ya kusawazisha bao hilo bado Tottenham walionekana kuongeza kasi na kutafuta bao la kuongoza, waliweza kufanya hivyo dakika nne baada ya kusawazisha, bao likifungwa na Henry Kane kwa mkwaju wa penalti baada ya Son Heung-min kuchezewa vibaya katika eneo la hatari.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Arsenal wakionesha mipango ya kutafuta bao la kusawazisha, waliweza kufanya hivyo katika dakika ya 56 Aubameyang aliandika bao la pili baada ya kupokea pasi kutoka kwa Aaron Ramsey ambaye aliingia kuchukua nafasi ya Henrikh Mkhitaryan.

Hata hivyo Arsenal walionekana kuwa kwenye ubora wao, waliweza kuongeza mabao mengine mawili ya haraka kupitia kwa nyota wao Alexandre Lacazette na Lucas Torreira.

Mchezo mwingine ulikuwa kati ya Chelsea ambao walikuwa kwenye uwanja wa nyumbani Stamford Bridge na kuweza kuutumia vizuri uwanja huo dhidi ya Fulham.

Chelsea walifanikiwa kupata bao la mapema sana katika dakika ya nne bao ambalo liliwekwa wavuni na mshambuliaji wake Pedro Rodriguez kutokana na kazi safi iliofanywa na kiungo wao N’Golo Kante.

Hata hivyo Fulham ambayo kwa sasa inasimamiwa na kocha mpya Claudio Ranieri, ilionekana kupambana kutafuta bao la kusawazisha lakini walishindwa kutumia nafasi walizozitengeneza.

Zikiwa zimesalia dakika nane mchezo huo kumalizika, Chelsea waliongeza bao la pili kupitia kwa mchezaji wao Ruben Loftus-Cheek baada ya Chelsea kupiga pasi kadhaa katika eneo la hatari la wapinzani.

Mchezo mwingine ulikuwa kati ya Liverpool ambao walikuwa kwenye uwanja wa nyumbani na kuwakaribisha wapinzani wao Everton, lakini hadi gazeti linakwenda mtamboni mchezo huo ulikuwa bado unaendelea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles