Imechapishwa: Fri, May 11th, 2018

ARIANA GRANDE, MILLER ‘WAMWAGANA’

NEW YORK, MAREKANI


STAA wa muziki na filamu nchini Marekani, Ariana Grande, amethibitisha kuachana na mpenzi wake wa muda mrefu rapa Mac Miller.

Wawili hao wamekuwa kwenye uhusiano tangu Septemba 2016, baada ya kuweka wazi uhusiano huo kwa mashabiki zao, lakini taarifa za kuachana kwao zilianza kusambaa tangu Jumatatu wiki hii.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ariana mwenye umri wa miaka 24, aliandika kwa sasa yupo singo na hana mpango wa kuingia kwenye uhusiano siku za hivi karibuni.

“Ni kipindi kigumu pale unapokuwa tofauti na yule ambaye ulikuwa unampenda, lakini kila kitu kina mwanzo na mwisho, natumia nafasi hii kuweka wazi kuwa sipo kwenye uhusiano na sina mpango wa kuwepo tena kwa kipindi cha hivi karibuni,” alisema mrembo huyo.

 

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

YOUTUBE

ARIANA GRANDE, MILLER ‘WAMWAGANA’