28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

‘ANKH CROSS’: MKUFU UNAOMTOA BOMBA DIAMOND NA MASTAA WAKUBWA DUNIANI

Na SWAGGAZ RIPOTA


 

HUWEZI kutenganisha fasheni na mastaa wa muziki wa kizazi kipya, kwani kupendeza ni jadi yao ya kudumu inayofanya waonekana nadhifu mbele ya hadhira. Kulipuka pamba za kileo na kuzinogesha kwa vipuli vya madini huongeza thamani ya biashara yao ya muziki.

Ndiyo maana tasnia ya mitindo duniani kote inategemea soko kutoka kwa wasanii wa muziki ambao wamekuwa kama kiunganishi cha wabunifu na wateja (mashabiki) wa bidhaa za mitindo kama vile mavazi na vifaa vya mapambo (pete na mikufu nk).

Moja ya wasanii wanaokwenda na wakati upande wa mitindo ni staa wa singo ya Hallelujah, (Diamond Platnumz) ambaye hivi sasa amekuwa akionekana na mavazi ya vitenge huku akishindilia mwonekano wake kwa mikufu na pete za thamani.

DIAMOND  APENDEZA  NA  ANKH

Hivi karibuni Diamond Platnumz amekuwa akionekana kuvaa mikufu mitatu kwa wakati mmoja ambayo ina umbo la msalaba ambao juu ya ule msalaba kuna duara fulani hivi. Kwa kimombo mkufu ule unaitwa Ankh Cross ambapo hapa Bongo ni wasanii wachache sana wamekuwa wakiuvaa kama vile Harmonize, Jux, Rich Mavoko.

Juma3tata leo tunakujuza mambo kadhaa ambayo huwenda ulikuwa huyajui kuhusu mkufu huo wa gharama ambao huvaliwa na mastaa wakubwa duniani kama vile Meek Mill, Dj Khaled, Rihanna, Rick Ross, Tyga, Beyonce na wengine wengi.

ASILI YAKE

Mwonekano wa mkufu huo unafanana na michoro inayopatikana kwa wingi kwenye mapango ya kihistoria ya miungu ya Misri iliyochorwa miaka 2000 iliyopita ikiwa na maana nyingi tata za kiimani.

Michoro hiyo ambayo imefanya mkufu wa Ankh upate umaarufu duniani kote, ndani ya mapango ya Misri ulikuwa na maana ya maisha ya ndani ya mtu binafsi.

Lakini pia humaanisha miungu ya maisha baada ya haya ya duniani na  mizumu kumpa mtu maisha kama zawadi kutoka kwa wafu na wakati mwingine ilipewa jina la Crux Ansata na ufunguo wa mto Nile.

TAFRISI  NYINGINE

Kwa mujibu wa mtandao wa Wikipedia, alama ya mkufu huo ina maana ya maisha ndani ya familia huku lile duara la juu likibeba maana ya mwanamke. Ule mstari wa chini umebeba maana ya mwanamume na ile mistari ya kushoto na kulia ina maana ya mtoto/watoto.

BEI ZAKE

Kama nilivyokwambia hapo awali kuwa mkufu wa Ankh umeonekana kuvaliwa zaidi na mastaa wakubwa duniani hivyo hata upatikanaji wake siyo wa kawaida. Juma3tata limekutana na duka linalouza mikufu hiyo kwa njia ya mtandao linaloitwa The GLD lenye makao yake nchini Marekani .

Thamani ya mkufu huo hutofautina kulingana na aina ya madini na uzito kwani kuna mikufu iliyotengenezwa kwa Almasi, Dhahabu na Shaba yenye uzito na mapambo tofauti.

Mfano mkufu mdogo wa Ankh wenye uzito wa gramu 5.5, uliotengenezwa kwa dhahabu na kunyunyiziwa dini la almasi kidogo huuzwa kwa dola 65  za Kimarekani ambazo ni sawa na shilingi 144, 224.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles