25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Anayedaiwa kutaka kumpindua Waziri Mkuu Ethiopia akimbia

ADIS ABABA-ETHIOPIA

ANAYETUHUMIWA kuongoza jaribio la kumpindua Waziri Mkuu wa Ethiopia , Dk. Abiy Ahmed sasa anasakwa kwa udi na uvumba na vyombo vya usalama vya nchi hiyo.

Ofisa wa ngazi za juu wa idara ya usalama alilithibitishia Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC,kwamba mtu huyo anasakwa.

aafisa wanne, akiwemo mkuu wa jeshi, waliuawa wakati wakizuia mapinduzi hayo.

Jana bendera zilikuwa zikipepea nusu mlingoti baada ya serikali kutangaza kuwa siku ya maombolezo.

Waziri Mkuu Abiy Ahmed ametoa wito kwa raia wa Ethiopia kuungana dhidi ya nguvu za ”kishetani” zenye nia ya kuigawa nchi yao.

Tayari vikosi vinavyounga mkono serikali vimepelekwa makao makuu ya mji wa Amhara, ambako mkuu wake wa usalama, Brigedia Jenerali Asaminew Tsige anashutumiwa kupanga mapinduzi hayo.

Aidha vikosi vingine vimepelekwa katika miji ya Bahir Dar, na mji mkuu Addis Ababa.

Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na mapigano Amhara na maeneo mengine ya Ethiopia.

Serikali ya Marekani imetahadharisha wafanyakazi wake mjini Addis Ababa kubaki majumbani.

Tangu kuchaguliwa kwake mwaka jana, Abiy amekuwa na nia ya kumaliza mivutano ya kisiasa kwa kuwaacha huru wafungwa wa kisiasa, kuondoa marufuku dhidi ya vyama vya siasa na kuwashtaki maafisa wanaoshutumiwa kukiuka haki za binadamu.

Ethiopia ni nchi ya pili yenye watu wengi barani Afrika (baada ya Nigeria), ikiwa na watu milioni 102.5 wa makabila zaidi ya 80.

Ni miongoni mwa nchi ambazo uchumi wake unakua kwa kasi , lakini idadi kubwa ya vijana nchini Ethiopia hawana ajira.

ANAYESHUTUMIWA KUPANGA MAPINDUZI

Ofisi ya Waziri Mkuu Abiy imemshutumu Asaminew kwa kupanga mapinduzi na Makamu wa idara ya usalama Amhara,  Gedebe Hailu aliiambia BBC kuwa kiongozi huyo hajulikani alipo.

Brigedia Jenerali Asaminew ni miongoni mwa maofisa wa juu wa jeshi walioachiwa huru mwanzoni mwa mwaka jana baada ya serikali iliyopita kuwaachia wafungwa wa kisiasa kutokana na msukumo kutoka kwa Umma.

Jenerali Asaminew amekuwa gerezani kwa miaka tisa akishutumiwa kupaga mapinduzi.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Uingereza, Reuters, maafisa wa juu wa Amhara walifanya mkutano siku ya Jumamosi kujadili majaribio ya jenerali ya kuwasajili wanamgambo.

Brigedia Jenerali Asaminew kwa wazi kabisa aliwashauri watu wa Amhara mwezi huu kujihami kwa silaha, katika video iliyosambaa kwenye mtandao wa Facebook na kushuhudiwa na mwanahabari wa Reuters.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles