Amber Rose: Nitazulula hadi siku ya mwisho

0
397

NEW YORK, MAREKANI

BILA ya kujali tumbo kuwa kubwa, mwanamitindo maarufu nchini Marekani, Amber Rose, ameweka wazi kuwa, ataendelea kuzulula hadi siku ya mwisho.

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 35, anatarajia kupata mtoto Oktoba mwaka huu, hivyo tumbo lake linaonekana kuwa kubwa kutokana na miezi ya ujauzito wake, lakini kila kukicha anaonekana akiwa mitaani.

Mrembo huyo ameweka wazi kuwa, ataendelea kutembea mitaani bila ya kujali ukubwa wa tumbo lake kwa kuwa hawezi kuzuia.

“Siwezi kutumia muda wote kulala kutokana na hali niliyonayo, nitaendelea kuwa mitaani hadi siku ya mwisho au hali yangu ikiwa tofauti, lakini kwa sasa hakuna tatizo,” alisema mrembo huyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here