33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Alliance yawekea rekodi uwanja wa Nyamagana

NA DAMIAN MASYENENE, MWANZA

Timu ya Alliance FC kutoka Jijini Mwaza imeweka rekodi ya kipekee kwenye Uwanja wa Nyamagana kakika michezo yake ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kucheza michezo 13 wakishinda 10 na sare tatu na kuandikisha historia ya kutopoteza mchezo kwenye dimba hilo la nyasi bandia.

Kama wanavyofahamika vyema vijana hao ni machachari wakiwa kwenye nyasi bandia na huwa wanapata wakati mgumu wakiwa kwenye viwanja vya kawaida, ambapo michezo yao pekee waliyopoteza nyumbani ni ile waliyotumia Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza ambapo walicheza mechi tano, wakapoteza minne na sare moja wakiwa hawana ushindi kwenye uwanja huo.

Alliance FC imecheza jumla ya michezo 37 imeshinda 10 nyumbani, miwili ugenini na sare saba, wamefugwa michezo minne ya nyumbani na 11 ya ugenini, jumla wameshinda michezo 12, sare saba na vichapo 15.

Michezo ya nyumbani waliyopoteza katika dimba la CCM Kirumba ni dhidi ya Simba 2-0, Yanga 1-0, Azam 1-0 na Mbao FC 1-0, na sare ya 1-1 dhidi ya African Lyon, huku sare tatu walizopata kwenye dimba la Nyamagana ni 2-2 dhidi ya Tanzania Prisons, 1-1 na Coastal Union na 2-2 dhidi ya Kagera Sugar.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Malale Hamsini tangu alipoiongoza timu hiyo kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Kagera Sugar na kukubali kichapo cha bao 1-0 alipojiunga nayo akitokea Ndanda FC ameiwezesha Alliance FC kusalia kwenye ligi msimu ujao baada ya kufikisha alama 47 katika nafasi ya tisa baada ya kushuka dimbani mara 37.

Malale alisema rekodi aliyoiweka ya kutopoteza mchezo wowote kwenye Uwanja wa Nyamagana ni ya kujivunia na kupongezwa kuanzia wachezaji waliojituma na kusikiliza maelekezo na mbinu kutoka benchi la ufundi pamoja na viongozi walioshiriki kutimiza mahitaji ya timu na wadau mbalimbali.

“Kila mchezo wa nyumbani tuliuchukulia kama fainali, tunashukuru tumetimiza lengo wachezaji wamepambana sana, hii rekodi kwa kweli ni ya kutia matumaini, naamini msimu ujao tutaendeleza hii historia,” amesema Malale.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles