24.4 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

ALIYEKUWA M’NYEKITI CCM IRINGA AKAMATWA

NA  FRANCIS  GODWIN


ALIYEKUWA  Mwenyekiti  wa CCM Mkoa  wa  Iringa, aliyefukuzwa  uanachama  kwa  usaliti  wakati  wa  uchaguzi  mkuu mwaka  2015, Dk.  Jesca  Msambatavangu, amekamatwa  na  Jeshi la  Polisi  kwa  tuhuma  za kumvamia  mwanamke  mmoja na  kumfanyia vitendo  vya  kinyama.

Moja ya kitendo kinachodaiwa kufanywa na Jesca, ni kumchoma mwanamke huyo sindano inayodhaniwa  kuwa  ya  sumu.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kamanda  wa Polisi  Mkoa  wa Iringa, Julius Mjengi, alisema Jesca alikamatwa  jana mchana, baada ya jeshi hilo kupokea taarifa ya tukio.

 “Tunamshikilia  Jesca  Msambatavangu  kwa  tuhuma  za  kumvamia na  kumpiga mwanamke  mmoja wa  kibwabwa katika Manispaa ya  Iringa.

“Inaonekana mwanamke huyu ameumizwa sehemu mbalimbali za mwili wake na inadaiwa walimchoma  sindano  inayodhaniwa  kuwa ya sumu,”alisema Kamanda Mjengi.

Alisema  mwanamke   huyo,  jina lake  limehifadhiwa kwa sababu za kiusalama, alivamiwa na watu  wanne  akiwemo Jesca.

Alisema  mpaka sasa wanaendelea na msako mkali  wa  kuwasaka watuhumiwa wengine  watatu ambao (majina  yao  yamehifadhiwa), kwa sababu wanadaiwa kuhusika katika   tukio  hilo.

“Tunawaomba wananchi wa mkoa huu, watoe ushirikiano wa kuwafichua watu hawa haraka ili wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria, hatuwezi kukubali matukio ya aina hii yaendelee katika jamii yetu,”alisema.

Itakumbukwa kuwa baada ya kufukuzwa uongozi na vikao vya juu vya CCM, Jesca alitangaza kutojihusisha tena shughuli zozote za siasa kwa  kuwa yote  yaliyotendeka  ndani  ya  chama chake, amemwachia  Mungu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles