33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

ALIYEBAKWA, MBAKAJI WAKE WASHIRIKIANA KUTUNGA KITABU

SI jambo rahisi lakini ndivyo ilivyotokea baada ya mwathirika wa kitendo cha ubakaji na mbakaji wake kukaa na kuandika kitabu pamoja kusaidia watu waliopitia katika hali kama hiyo kutengeneza amani.

Wawili hao Thordis Elva na Tom Stranger, wameandika kitabu kinachoenda kwa jina South of Forgiveness.

Walikutana katika kipindi kimoja cha runinga cha TED Talk nchini Marekani na kuzungumzia kisa hicho katika safari yao ndefu ya maridhiano.

Kwa mujibu wa tovuti ya Stuff, Stranger kutoka Australia akiwa na umri wa miaka 18 alisafiri kwenda Iceland kama sehemu ya program ya kielimu ya kubadilishana wanafunzi baina ya mataifa hayo mwaka 1996.

Akiwa huko alikutana na Elva aliyekuwa na  umri wa miaka 16 wakati huo, ambapo walijenga urafiki baina ya mvulana na msichana kabla ya siku moja kwenda kwenye muziki kusherehekea Sikukuu ya Krismasi.

Hata hivyo, baada ya muziki huo maalumu kwa wanafunzi shuleni, Stranger alimbaka Elva aliyekuwa hajitambui kutokana na ulevi.

Baada ya Tom kumbaka Thordis, wawili hao walitengana kwa miaka mingi, maana Tom alirudi kwao baada ya kumalizika kwa program yake hiyo.

Katika jaribio la kutaka kufahamu athari za kilichotokea, Thordis, ambaye sasa ana miaka 36, aliamua kumsaka rafikiye huyo wa zamani wa kiume na sasa wameaandika kitabu pamoja.

Kupitia hadithi hiyo, wawili hao wanatafuta namna ya kukabiliana na ukatili wa kijinsia unaoshuhudiwa kote duniani kupitia kitabu hicho.

Baada ya dansi, Elva ambaye kwa sasa ni mwandishi na mtaalamu wa maandishi nchini Iceland hakuwa anajitambua baada ya kulewa chakari na Stranger akampeleka nyumbani kwake. “Alinilaza kitandani!

Shukrani niliyokuwa nayo kwake ya kumruhusu anipeleke nyumbani kwangu iligeuka mateke na ukatili mkubwa kwa sababu alinivua nguo zote na kunitendea uovu,” Elva alisema katika kipindi hicho kilichokuwa maalumu kusherehekea Siku ya Kimataifa ya wanawake mapema mwezi uliopita. 

Licha ya kuchechemea siku kadhaa na kujikuta akilia kwa majuma mengi, Elva anaeleza kuwa ilimchukua miaka mingi kutambua kuwa alikuwa amebakwa.

“Kitu ambacho kingenizuia kubakwa usiku huo ni mwanamume, ambaye alinibaka – kama angejizuia kufanya tendo hilo.”

Tukio hilo lilifanywa na Stranger, ambaye kwa sasa pia ni mwandishi na mtaalamu wa saikolojia mjini Sydney, pia akiwa bado hajafikisha umri wa miaka 20. Hakuona kama tendo lake hilo lilikuwa kosa.

“Neno ‘ubakaji’ halikuwa akilini mwangu. Sikukubali kuwa ilikuwa kosa nikijishawishi kuwa tulifanya mapenzi na wala sio tendo la ubakaji. Na huu ni uongo, ambao nimekuwa nikiishi nao kwa miaka mingi.”

Ilichukua Elva miaka tisa kutokubali na kukimbia huku na huko, kutambua kilichokuwa kikimsumbua maishani.

Alimuandikia Stranger barua kumweleza kitendo alichomfanyia. Barua hiyo ilianzisha mawasiliano ya miaka minane kati yao kupitia mtandao.

Hata hivyo, hakupata suluhu. Kwa hiyo, wawili hao walikutana mjini Cape Town nchini Afrika Kusini, ambako walizungumzia kwa kina tukio hilo ana kwa ana.”

Wawilio hao wanaamini kitabu chao hicho kitasaidia katika maridhiano kati ya mbakaji na aliyebakwa. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles