Imechapishwa: Wed, Jan 3rd, 2018

ALI KIBA ATIKISA KIGALI

NA BRIGHITER MASAKI


STAA wa Bongo Fleva, Ali Kiba, juzi alitikisa Jiji la Kigali nchini Rwanda kwa kufanya tamasha kali la kufungua mwaka.

Tamasha hilo la ‘East African Party 10’ ambalo lilifanyika katika Uwanja wa Taifa wa mpira wa miguu nchini Rwanda maarufu kama Amahoro, Ali Kiba alijaza watu kwenye uwanja huo.

Ali Kiba alitumbuiza nyimbo zake nyingi za zamani ikiwemo Mac Muga, Cinderella, Nakshi Mrembo na wimbo wake mpya ukiwemo Sedece Me.

Mkali huyo ambaye hivi karibuni aliomba radhi kwa mashabiki zake nchini kwa kutokufanya tamasha la Funga mwaka na Kiba, hatimaye amefungua mwaka nchini Rwanda na kukosha nyoyo za mashabiki wake.

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

YOUTUBE

ALI KIBA ATIKISA KIGALI