23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Al-Shabab waua watu sita Kenya

ali-robaMOMBASA, KENYA

WATU sita wameuawa baada ya wanamgambo wa Al-Shabab kushambulia mitaa ya Jimbo la Mandera, kaskazini mashariki mwa Kenya.

Taarifa zinasema washambuliaji hao kutoka Somalia walivamia eneo lenye nyumba za makazi la Bulla usiku wa kuamkia jana.

Gavana wa Jimbo hilo, Ali Roba, ameandika kwenye mtandao wa Twitter kwamba watu sita wameuawa na mmoja kujeruhiwa.

Amesema watu 27 kati ya 33 waliokuwa eneo hilo wameokolewa na maofisa wa usalama.

Kituo kimoja cha redio kinachohusishwa na kundi la Al-Shabab kimesema wanamgambo hao walitekeleza shambulio hilo.

Gazeti la Daily Nation la hapa limeripoti kuwa watu walioshambuliwa walitokea  maeneo mengine.

Aidha, Gazeti la Standard nalo linasema walioshambuliwa walirusha guruneti kisha wakaingia ndani na kufyatua risasi kwa waliokuwemo.

Eneo la Mandera limekuwa likishambuliwa mara kwa mara na wapiganaji hao.

Kenya ilipeleka vikosi vyake nchini Somalia mwaka 2011, ikitaka kuzima mashambulizi ya mara kwa mara na kuisaidia Serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.

Kundi la Al-Shabab mara kwa mara hutekeleza mashambulizi nchini Kenya ikiwemo mauaji ya watu 67 katika maduka ya Westgate mjini Nairobi mwaka wa 2013.

Juni mwaka huu, wanamgambo hao walishambulia gari ya polisi aina ya Land Cruiser, kilomita chache kutoka Mji wa Mandera na kuua maofisa watano wa polisi.

Mwaka uliopita Al-Shabab walitekeleza mashambulizi katika Chuo Kikuu cha Garissa na kusababisha vifo vya wanafunzi 148.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles