30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Al Shabab waua maofisa saba wa polisi, daktari mmoja Kenya

WAJIR, KENYA

MAOFISA saba wa polisi na daktari mmoja ni miongoni mwa watu 10 waliouawa na wapiganaji wa kundi al-Shabab waliotekeleza shambulio kwenye basi moja la abiria katika kaunti ya Wajir. 

Wapiganaji wa Al Shabab wamekuwa wakitekeleza mashambulizi ya mara kwa mara katika eneo la kaskazini mwa Kenya

Askari hao wamedaiwa kutoka katika kitengo cha Anti-stock huku utambulisho wa raia wengine wawili waliouawa ukiwa haujulikani.

Walioshuhudia tukio hilo wameliambioa Shirika la Utangazaji la Uingereza la BBC kwamba wapiganaji kadhaa waliokuwa wamejihami walishambulia basi hilo lililokuwa likielekea Mandera na kuwalenga watu wasiotoka katika eneo hilo baada ya kuwatenga kutoka kwa abiria wengine.

Kisa hicho kinadaiwa kufanyika kati ya miji ya Wargadadud na Kutulo.

Kulingana na gazeti la Daily Nation nchini Kenya, kamanda wa polisi katika kaunti hiyo, Stephen Ngetich amethibitisha tukio hilo lakini hakuweza kutoa idadi kamili ya walioathiriwa.

Ngetich amesema kwamba kikosi cha maofisa maalum tayari kimetumwa katika eneo hilo.

”Naweza kuthibitisha kwamba kundi moja la watu waliojihami walishambulia basi ambalo lilikuwa linaelekea Mandera siku ya Ijumaa jioni ijapokuwa bado hatujapata habari kamili kuhusu idadi ya waliouawa”, alinukuliwa akizungumza na gazeti la Daily Nation.

Basi hilo la Madina linadaiwa kushambuliwa juzi saa kumi na moja jioni.

Shambulio hilo linajiri mwezi mmoja baada ya wapiganaji wa al-Shabab kushambulia kituo cha polisi cha Wajir katika jaribio la kutaka kuwaachilia huru washukiwa wawili wa ugaidi ambao walikuwa wanazuiliwa katika kituo hicho.

Kundi la wapiganaji wa al-Shabab nchini Somalia ambalo limekuwa likitekeleza mashambulio hayo mara kwa mara katika eneo hilo limekiri kutekeleza shambulio hilo likisema kuwa limewaua takriban watu 10.

Katika taarifa iliyochapishwa katika mojawapo ya tovuti zake, kundi hilo linasema liliwalenga abiria wasiokuwa Waislamu katika basi hilo.

Kisa hiki kimetokea katika barabara ambayo takriban Wakenya 28 waliokuwa wakisubiri basi moja walishambuliwa na kuuawa miaka mitano iliyopita.

Barabara hiyo ipo karibu na mpaka wa Somalia.

WALIOANGUKIWA NA GHOROFA 

Wakati huo huo, watu waliofariki baada ya jengo la ghorofa sita kuporomoka Kenya wamefikia watano.

 Jengo hilo lililokuwa likikaliwa na familia 46 lilianguka siku ya Ijumaa asubuhi katika eneo la Embakasi jijini Nairobi.

Mbali na watu hao watano, wengine kadhaa wanahofiwa kunaswa chini ya kifusi cha jengo hilo.

Shughuli za uokoaji zinaendelea. Ripoti zinasema watu kadhaa wameokolewa na kukimbizwa hospitalini kwa ajili ya matibabu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles