31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Al-Shabab 142 wauawa

MOGADISHU, SOMALIA

JESHI la Somalia (SNA) limetangaza kuwa limewaua magaidi wapatao 142 wa kundi la al-Shabaab, kuwajeruhi 29 na wengine 18 wamekamatwa kwenye operesheni iliyofanyika katika mji wa Janale, kusini mwa Somalia.

Kamanda wa jeshi hilo, Osman Shabel alisema wanajeshi waliukomboa tena mji wa Janale kutoka kwa magaidi hao wakufurishaji wenye mfungamano na al-Qaeda wiki mbili zilizopita.

Aliongeza kwamba hakuna majeruhi kwa jeshi la Somalia, na wanajeshi hao walizirejesha familia zilizoondolewa kwenye nyumba na kuwapa chakula.

Jeshi la Somalia limekuwa likiwalenga magaidi wa Al-Shabaab katika eneo la Lower Shabelle katika kipindi cha wiki mbili zilizopita.

Siku chache zilizopita, magaidi 12 wa  al-Shabaab waliangamizwa katika operesheni ya jeshi la Somalia katika eneo la Bay, Kusini mwa nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.

Haya yanajiri siku tatu baada ya vikosi vya jeshi la Serikali vikishirikiana na askari wa Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Afrika nchini humo (Amisom) kuua magaidi sita wa al-Shabaab katika operesheni dhidi ya maficho ya magaidi hao katika vijiji vya eneo la Lower Juba, Kusini mwa nchi.

Kundi la kigaidi la al-Shabaab lenye mfungamano na mtandao wa al Qaida limekuwa likifanya mashambulizi ndani ya Somalia kwa lengo la kuiangusha Serikali kuu ya nchi hiyo inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.

Umoja wa Mataifa unafadhili askari hao wa Amisom ambao sasa ni 21,000 na wamekuweko nchini Somalia tokea mwaka 2007. Wanajeshi wa Amisom walioko Somalia ni kutoka Uganda, Kenya, Burundi, Somalia, Ethiopia, Djibouti na Sierra Leone.

Nao maofisa wa polisi wa AMISOM ni kutoka Nigeria, Sierra Leone na Uganda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles