24.4 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

AKOTHEE: NAKOSA UHURU KUKAA NA MWANAMUME

NAIROBI, KENYA


NYOTA wa muziki nchini Kenya, Esther Akothee, amefunguka na kusema kuwa, hawezi kukaa na mwanamume kwa kuwa anaamini atakosa uhuru wa kufanya kile akitakacho.

Mrembo huyo hadi sasa anaishi mwenyewe na watoto wake watano, ambao wana baba tofauti, ametumia ukurasa wake wa Instagram kuwaeleza mashabiki wake kwamba hana mpango wa kukaa na mwanamume.

“Furaha ambayo ninayo kwa sasa nataka watoto wangu wote waipate wakiwa kwenye mikono yangu, lakini ninaamini kama nitaamua kukaa na mwanamume basi watoto hao watakosa furaha ninayoitaka.

“Hata hivyo, ni wazi kwamba ninahitaji uhuru wa kufanya mambo yangu niyatakayo kwa wakati wowote, lakini nikiwa na mwanamume itakuwa ngumu kufanya baadhi ya mambo,” alisema Akothee.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles