23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Ajib amtega Omog

MSHAMBULIAJI wa Simba, Ibrahim Ajib
MSHAMBULIAJI wa Simba, Ibrahim Ajib

Na MOHAMED KASSARA-DAR ES SALAAM

MSHAMBULIAJI wa Simba, Ibrahim Ajib, amemtega Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mcameroon Joseph Omog, akidai kuwa hatima yake ndani ya klabu hiyo ipo mikononi mwake, endapo ataamua kumchezesha kikosi cha kwanza katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Ajib, ambaye amebakiza miezi sita kumaliza mkataba wake na Simba, hafurahishwi na kitendo cha kuwekwa benchi na kupangwa kucheza kipindi cha pili, huku akianzishwa kiungo, Mohamed Ibrahim, aliyetokea Mtibwa Sugar.

Akizungumza na MTANZANIA jana, straika huyo aliyefunga mabao manne msimu huu, alisema amejifua vya kutosha katika kipindi cha mapumziko wakati ligi ikiwa imesimama ili kuhakikisha anapata namba kikosi cha kwanza kwenye duru ya pili.

“Nikipewa nafasi nitafanya vizuri, lakini sijui mwalimu Omog ataanza vipi mzunguko wa pili ambao ninaamini kila mchezaji atakuwa amejipanga kuhakikisha anakuwa sehemu ya kikosi cha kwanza,” alisema.

Aidha, Ajib alisema Simba bado ina nafasi kubwa ya kunyakua ubingwa wa ligi kuu msimu huu, kwani ndiyo timu inayoongoza kwenye msimamo kwa kujikusanyia pointi 35, licha ya kupoteza michezo miwili ya mwisho katika mzunguko wa kwanza.

“Tutarudi kivingine kuhakikisha tunaendelea kufanya vizuri na kufikia malengo ya kuchukua ubingwa, ingawa tulianza vizuri duru ya kwanza na kasi yetu kupungua mwishoni,” alisema Ajib.

Hadi sasa straika huyo bado hajafanya uamuzi kama ataongeza mkataba mwingine Simba, licha ya viongozi wa klabu hiyo kuendelea kuhangaika na kufanya juhudi za kumbakisha katika kikosi hicho.

Hata hivyo, Ajib huenda akaondoka Simba baada ya mkataba wake kumalizika, kutokana na kukosa namba kikosi cha kwanza katika mechi za mwishoni mwa duru ya kwanza ya ligi.

Simba tayari imemwongezea mkataba wa miaka miwili beki wake wa kushoto, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ katika usajili wa dirisha dogo, baada ya kushtukia ujanja wa mahasimu wao, Yanga waliokuwa wakimuwinda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles