31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

AJALI YAUA SABA KIGOMA

Na Editha Karlo, Kigoma

Watu saba wamefariki dunia katika ajali ya gari aina ya Scania iliyotokea katika Kijiji cha Mkongoro, Barabara ya Manyovu Wilaya ya Kigoma Vijijini.

Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma, Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva kushindwa kuimudu gari kwenye mteremko.

Amesema ajali hiyo imetokea leo Jumatano Machi 21, saa tatu asubuhi katika Mlima wa Kasagamba ambapo lori lenye namba T741AAB  lilianguka na kusababisha vifo vya watu saba akiwamo dereva wa gari hiyo aliyefahamika kwa jina la Siri Hamis (43) mkazi wa Singida pamoja na utingo wake aliyefahamika kama Ramadhani Saidi (23).

“Katika gari hiyo walikuwa wamebeba mizigo na watu wanne mmoja mwanamke na watatu wanamume ambapo wengine waliofariki na majina yao hayakufahamika mara moja.

“Ajali hiyo pia imesababisha kifo cha mwanafunzi aliyefahamika kwa jina la Eliakimu Samsoni (15 ), aliyekuwa akitembea kwa miguu kuelekea shuleni na gari hilo kumgonga akiwa anatembea,” amesema Kamanda Otieno.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles