25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Ajali ya basi yaua sita Ipogolo

pic+kamandaNA RAYMOND MINJA, IRINGA

WATU sita wamefariki dunia papo hapo na wengine zaidi ya 38 kujeruhiwa  vibaya,baada ya basi walilokuwa wakisafirika kutoka Mwanza kwenda mkoani Iringa kupinduka juzi usiku.

Basi hilo  lilipinduka katika eneo lenye mteremko mkali la Ipogolo baada ya dereva kushindwa kulimudu.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa,Peter Kakamba alisema jana kuwa ajali hiyo ilitokea juzi saa 3:30 usiku baada ya basi la Lupondije la Scania   mali ya Lupondije Express    kupinduka  eneo la  mteremko  wa Ipogolo   lilipokuwa  likielekea  kushusha abiria  wa kwenda   mkoani Mbeya.

Alisema majeruhi 38 walifikishwa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa na 11walitibiwa na kuruhusiwa, wakati 27 hali zao hazikuwa nzuri.

Mmoja wa abiria  kwenye basi hilo, Wema  Zuberi alisema  mwendo  wa basi hilo tangu linaondoka mkoani Dodoma ulikuwa wa kawaida.

Alisema baada ya  kuingia  Iringa mjini, dereva  wa basi  hilo alianza kuendesha kwa mwendo kasi na kusababisha abiria kulalamikia mwendo huo.

“Abiria  wengi  walionyesha  kumlalamikia  dereva kutokana na  kuwapitisha vituoni  kuwashusha huku akiendesha mwendo kasi,”alisema.

Alisema kabla ya  kufika  eneo  la ajali ,dereva alishindwa kulimudu basi hilo kutokana na mteremko  mkali, huku breki zake zikishindwa kufanya kazi.

Aliwataja waliojeruhiwa  kuwa ni Banenda Helen (45), Mbuyi Leoni (52) wote raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Jojina Nyamboko (26) mkazi wa Songea,Magambo Masunga (51) mkazi wa Mwanza,Felister Mwinuka (19) mkazi wa Njombe, Tubilisiusy Selestine(33),Said Kitonyi (17),Richard Bett (33) raia wa Kenya na Jofa Abonga (30)mkazi wa Geita.

Wengine  ni Victor Lameck (25), mkazi wa Kagera, Pius Samwel (20) mkazi wa Mara, Michael Hadu (46) mkazi wa Madaba Songea, Hassan Mfaume (20) kutoka Iringa, Heriet Mwitinda (29) mkazi wa Arusha, Kiliana Kalinga

(22) mkazi wa Mbeya, Hima Kifyasi (32) mkazi wa Bariadi, Omary Hassan (35) mkazi wa Makambako,Zuo Pawa (30) mkazi wa Mbeya, Chacha John (26) kutoka Iringa.

Wengine  ni Timoth Sichoni (24) mkazi wa Dodoma, Ishimwe Jasmin (9) raia wa Rwanda, Mkagasana Sarafina (41) raia wa Rwanda, Zaina Kisaka (26) mkazi wa Manyara, Sara Sichone (26) mkazi wa Mwanza, Ivon Magaiwa (22)mkazi wa Mafinga, Solomoni Angolisye (58) mkazi wa Dodoma, Ivan Huwen (33) na mwingine ambaye hajatambuliwa kutokana na hali yake kuwa mbaya.

Alisema baada ya kutokea ajali hiyo  dereva alikimbia.

Akizungumza eneo la tukio, Mkuu  wa  wilaya ya  Iringa,Richard Kasesela alisema  kazi ya     kutafuta  miili zaidi iliyobanwa na basi  hilo imekuwa  ngumu  kutokana na kukosekana gari la kuinua  basi hilo.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Robert Salim alikiri kupokea miili ya marehemu sita na majeruhi 38.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles